Tanzania ilivyojipanga kudhibiti uvujaji mitihani ya utabibu

May 31, 2022 7:44 am · David
Share
Tweet
Copy Link
  • Kuboresha mifumo ya usimamizi wa mitihani.
  • Kuunda mamlaka kamili ya kusimamia mafunzo ya vyuo vya afya.

Dar es Salaam. Baada ya Serikali ya Tanzania kukiri kuvuja kwa mitihani ya utabibu ngazi ya stashahada, imesema itaimarisha mifumo yake ya usimamizi katika ngazi zote ili kuhakikisha vitendo hivyo havijirudii tena.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga ametoa kauli hiyo leo Mei 31, 2022 jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Husna Sekiboko aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu kuvuja kwa mitihani hiyo.

“Nini ni kauli ya Serikali juu ya kuvuja kwa inayosimamiwa na vyuo vya afya 2021,” ameuliza Sekiboko.

Akijibu swali hilo, Kipanga amesema kuwa Serikali itaboresha mifumo ya uchapishaji na ufungaji wa mitihani, kufanya mapitio ya miongozo ya mitihani iliyo chini ya Wizara ya Afya ili kuendana na mahitaji ya ulinzi na kiusalama.

Pia itaanzishwa mamlaka itakayayosimamia mafunzo ya vyuo vya afya ngazi ya kati pamoja na uendeshaji wa mitihani.

                                

Oktoba mwaka jana, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte) lilizuia matokeo ya mitihani ya utabibu ngazi ya stashahada ikisubiri uchunguzi unaofanywa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto kutokana na kuvuja kwa mitihani hiyo.

Mitihani hiyo iliyofanywa kati ya Agosti 12 na Septemba 11 mwaka jana katika vyuo 147 nchini, ilivuja kwa baadhi ya vyuo kuinunua.

Baadhi ya wabunge wamesema Serikali inapaswa kutoa adhabu kali kwa maafisa wote wa Wizara ya Afya waliohusika na uvujaji wa mitiani hiyo kama  ambavyo imekuwa ikifanya kwa shule za msingi na sekondari.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV