Serikali yapendekeza kuondoa ada vyuo vya ufundi Tanzania

June 16, 2023 4:50 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa ajili ya kuongeza wataalamu wenye ujuzi kuchochea mapinduzi ya viwanda.
  • Vyuo vinavyopendekezwa ni DIT, MUST, pamoja na ATC.

Dar es Salaam. Serikali inakusudia kuondoa ada katika ngazi ya elimu ya kati kwa baadhi ya vyuo vya umma nchini ili kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi unaohitajika katika mapinduzi ya viwanda yanayotarajiwa kuwa gurudumu la uchumi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amewaambia wabunge jijini Dodoma kuwa katika jitihada za kuondoa ada kwa wanafunzi nchini anapendekeza sasa kuwaondolea karo wanafunzi watakaochaguliwa na Serikali kujiunga vyuo vya ufundi. 

Katika hotuba yake ya bajeti, Dk Nchemba vyuo vinavyopendekezwa kufutiwa ada ni  Dar es Salaam Institute of Technology (DIT), Mbeya University of Science and Technology (MUST) pamoja na Arusha Technical College (ATC).

“Napendekeza kuondoa ada kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na kupangiwa na Serikali kujiunga na vyuo vya ufundi vya DIT, MUST  na ATC, hatua hii inalenga kuongeza idadi ya wataalamu wenye ujuzi na elimu inayohitajika katika azma hizi za mapinduzi ya nne ya viwanda,” amesema Dk Nchemba.


Soma zaidi


Kwa muda mrefu wadau wa mbalimbali wamekuwa wakiishauri Serikali kuondoa ada au kuweka utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya kati jambo ambalo Mwigulu amesema Serikali inakusudia kutekeleza mwaka 2023/24.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV