Serikali yaanza kuwanoa walimu kwa mafunzo ya amali

June 26, 2023 2:55 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni maandalizi ya utekelezaji wa mabadiliko ya Sera na mitaala ya elimu
  • walimu 506 wanaofundisha wenye  mahitaji maalumu kupata darasa kwa siku nne

Mwanza. Serikali imeanza kutekeleza mabadiliko ya Sera ya Elimu nchini kwa kutoa mafunzo ya amali kwa walimu ili kuwaandaa wanafunzi kuwa na uwezo wa kuajiriwa na kujiajiri pindi wamalizapo masomo yao.

Amali ni mafunzo yanayohusisha ujuzi wa ufundi na ufundi stadi katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufundi cherehani, makenika, uashi pamoja na ususi.

Pamoja na kumuwezesha mwanafunzi kufahamu stadi mbalimbali za maisha mafunzo hayo yanalenga kuwanoa wanafunzi katika lugha ili waweze kuzungumza na kuandika kwa ufasaha Kiingereza na Kiswahili.

Mkurugenzi wa idara ya Elimu nchini Huruma Elias, aliyekuwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa walimu 506 wanaofundisha wanafunzi wenye uhitaji maalumu amewaambia lengo la mafunzo hayo ni kuwapa ujuzi utakaowasaidia wahitimu kufanya shughuli za uzalishaji.

“Tuna mabadiliko ya sera na mitaala ambapo walimu watapatiwa mafunzo ambayo yata msaidia mtu aweze kujiajiri ambapo pamoja na mwalimu kuandaliwa kufundisha ualimu lakini awe na somo mojawapo la amali ambalo atalifundisha kwa wanafunzi,” amesema Elias

Mafunzo hayo ya siku nne yaliyohusisha walimu kutoka mikoa ya Mwanza, Kagera, Kigoma, Mara na Shinyanga ni mwendelezo wa mafunzo yaliyofanyika mwaka 2022.

Jumla ya halmashauri 144 zimeshapatiwa mafunzo hayo  ambapo walimu 39,000 wa Sekondari wameshapatiwa mafunzo hayo na wa shuke za msingi ni walimu 3,799.

Selemani Idrisa ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mkeza iliyopo Manispaa ya Bukoba amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati mwafaka hasa kwa walimu walioko kazini kwani yatamfanya mwalimu aendane na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia yaliyopo hivi sasa.

“Ni mafunzo ambayo yanaendana na wakati uliopo wa ukuaji wa teknolojia yatamfanya mwanafunzi awe wa kisasa zaidi ,”amesema Idrisa 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV