Sababu Lissu kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa

December 12, 2024 4:07 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na mabadiliko ya hali ya kisiasa, hitaji la mabadiliko pamoja na haki ya katiba ya Chadema.
  • Ataja kuimarisha demokrasia ndani ya chama pamoja na usimamizi wa rasilimali.
  • Mbowe asema uamuzi wa kugombea au kutogombea utatokana na wanachama wa Chadema.

Dar es Salaam.Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tanzania Bara Tundu Lissu ametangaza rasmi nia ya kugombea uenyekiti wa chama hicho akieleza kuwa mabadiliko ya hali ya kisiasa, hitaji la mabadiliko pamoja na haki ya katiba vinamruhusu kugombea nafasi hiyo.

Lissu ambaye huenda atachuana na mwenyekiti wake wa sasa Freeman Mbowe aliyekalia kiti hicho kwa miongo miwili ametangaza uamuzi huo leo Desemba 12, 2024 katika mkutano wake na wanahabari jijini Dar es Salaam ambapo amesema ameshawasilisha rasmi kusudio la kuwania nafasi hiyo kwa Katibu Mkuu wa Chadema.

Katika mkutano huo makada wa chama hicho kutoka kanda zake nane, walionekana wakiwa wamebeba mabango yaliyoandikwa ‘Tundu Lissu ni yeye 2024/29 haki huinua Taifa.’

“Napenda kuwajulisheni rasmi kwamba nimeshawasilisha taarifa rasmi kwa katibu mkuu wa chama chetu ya kuondoa kusudio langu la kugombea nafasi ya makamu mwenyekiti kwa upande wa Tanganyika nililowasilisha tarehe 6 Agosti 2024 na badala yake sasa nimewasilisha kwa katibu mkuu kusudio rasmi la kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama taifa katika uchaguzi ujao,” amesema Lissu.

Lissu amesema ameamua kugombea nafasi hiyo ili kuweka mbinu mpya za kufanya siasa katika mazingira ya sasa, ikiwamo kuisuka upya Katiba ya Chadema na kuweka ukomo wa uongozi katika ngazi mbalimbali ndani ya chama hicho ikiwemo kwa wabunge wa viti maalum na madiwani.

“Chama chetu (Chadema) kimekuwa kikubwa sana. Hakuna tena hofu ya kukosa viongozi katika ngazi mbali mbali za uongozi wa chama. Michuano mikali ambayo tumeishuhudia katika chaguzi za chama zinazoendelea ni ushahidi tosha kwamba chama kimekua. 

Katika mazingira haya, hatuna budi kurudisha tena utaratibu wa kikatiba wa ukomo wa madaraka katika chama tuliokuwa nao katika miaka ya mwanzo ya chama chetu,” amesema Lissu.

Makamu Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani, Chadema, Tundu Lissu, akihutubia mkutano  wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Picha /Sunday  George /The Citizen.

Hata hivyo, Lissu ameongeza kuwa sababu nyingine ya kugombea ni kuhakikisha matakwa ya wanachama yanajibiwa ikiwa ni pamoja na kuunda mfumo mpya wa kusimamia chaguzi za ndani za chama hicho na kuweka utaratibu wa kupokea na kushughulikia rufani za wagombea waliokata rufaa akitolea mfano wa mfumo wa upigaji kura wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS).

Lissu amesisitiza kuwa bado kwenye chama chake  hakuna usimamizi bora wa rasilimali fedha ikiwemo utafutaji na mgawanyo wake kwa kanda, mikoa, wilaya na majimbo na ngazi za chini zaidi ambako shughuli nyingi za chama zinafanyika.

Aidha, Lissu amesema haikuwa rahisi kwake kufikia uamuzi wa kugombea nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho akiongeza kuwa tangu mwaka 2015 kulikuwa na vishawishi vya kumtaka awanie nafasi hiyo na hakuwa tayari na sasa amejipima ameona anafaa kuwania nafasi hiyo.

“Ninaamini na ninapenda kuamini ninyi wanachama wenzangu nina sifa za kutosha za kugombea nafasi ya juu kabisa ya chama chetu (Chadema) yaani nafasi ya mwenyekiti wa chama Taifa,” amesema Lissu.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akihutubia mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam .Picha / Chadema

Msimamo wa Mbowe 

Itakumbukwa Mbowe juzi Jumanne Desemba 10, 2024 akijibu swali aliloulizwa na mwanahabari kuhusu kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho wakati akitoa maazimio 11 ya chama chake baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, alisema uamuzi wa kugombea au kutogombea utatokana na wanachama wa Chadema.

“Ooh! wengine wanasema Mbowe umekaa sana miaka 20 ni hivi, miaka 20 ni ya kukomaa, hebu wewe jaribu kukomaa kwa miaka 20 fanya kazi uone komaa yako itakavyokuwa, mwingine analinganisha kwamba Nyerere (Julius) alinga’ tuka…

Nyerere alikuwa mtumishi wa umma, analipwa mshahara, hafungwi wala kushtakiwa, sisi unaona hapa wote tunajitolea. Miaka 20 ya kukomaa,” amesema

1 thought on “Sababu Lissu kugombea uenyekiti wa Chadema Taifa

  1. Naungana mchapidhaji wa hili jarida lakni pia hata katika hawa wanaosoma je mitaala yao inawajenga kwenda kuwa watalamu kamili? Kwamfano hawa Nurse Anaesthesia hawa watu wanasoma miaka mnne hii course lkn kwann mtaala wao hauna misingi iliyo bora kwanini hawapewi haki yao ya kiamasomo akati ni haki yao? Kwanini hawa watu wasifundishwe Pathology,Dissection Anatomy, Anatomy in anaesthesia? Badala yake hawa watu wanafundishwa maswala ya nursing for what purpose akati hawa ni physician kabisa?

    Hawa wanafunzi kila kukicha wanahudhulia katika mahofsi kufatilia hatima yao juu ya hii course lakini watoto wawakulima wanaosomeshwa kwa shida hata tu mtaala yani ambayo ni haki yao wananyimwa? Waliomba mtaala upitiwe upya serikali ikatoa bajeti ya emergency review of carculum na kuahidiwa kuwa nawao watakuwa kama wadau lakini imekuwa tofauti ni kwamba hawahusishwi katika chochote ndo kusema kwamba mtaala unapitishwa kisirisiri au imekaaje wakati hawa nao ni wadau moja kwa moja na ndo wahanga wenyewe?
    Kwanini shahada ilizinshwa mnamo mwaka 2019 huoo mpaka sasa hawa watu hawatambuliki hata kwenye mfumo wa utumishi Tanzania?
    Kwanini clical officers anaruhusiwa kusoma level ya certificate lkn ikifika bachelor huyu mtu haruhusiwi? Kwamb hii course ni ya watu binafsi sio watanzania wote kwamfano kwanini mwanafunzi huyuhuyu wa nursing akitokeq diploma akienda kusoma bacheloranao uwezo wakusoma physiotherapia, audiology, occupation therapy na nk kwanini kuhusu hii course kuna restriction kiasi hiki kwanini huyuhuyu CO anaeruhusiwa kusoma certificate bachelor haruhusiwi hii haiko sawa hata kidgo?
    Kwanini shahda hii ikaboreshwa na ikajisimamia yenyewe ili kufanya maboresho zaidi hasa katika utendaji Yani ikawa na foundation nzuri huku chini mpka juu yani certificate, diploma, bachelor ili hata hawa wanaosoma nje waingie humo humo kwasababu wanavigezo kwanini shahada inafanywa ni kama yawatu fulani,!!
    Wadau wa elimu au wabobezi zaidi kwanini hii course msiiwekee msingi tu mizuri kama hapo juu kwanini isiitwe bachelor in anaesthesia ili kumruhusu huyu CO na nurse mwenye vigezo tu aingie? Na kuboresha zaidi katika utendaji kuepusha kuingiliana katika mjukumu kwamfano ilivo sasa nurse Anaesthesia anaesoma miaka minne huyu mtu anasomeshwa uuguzi wanini while he/she is completely physicion wa usingzi hapa unamwandaa muuguzi au mtoa dawa za usingzi au ndo mtu nusu nusu kama ni kwamba ndio anaandaliwa nurse Anaesthesia kwann wasiendelee kutumika wauguzi tu waliopo ambao ni wengi wanazaliswa kila leo wengne hata hawana ajili harafu unakuja kumuandaa hata huyu mtoa dawa ambae he/she is not competent enough kuhusu anaesthesia ifike hatua Tanzania tuondoe siasa kwenye vitu nyeti kama hivi yani binafsi najiuliza kwann huyu mtu anaeenda kumlanza mgonjwa katika operation haumfundishi Dissection Anatomy ili akaone zile nerves zote vizuri awe complent na zikamsaidie katika utendaji??
    Ukipitia mitaala ya nchi za wenzetu anaesthesia anasoma haya masomo na hata ukiangalia katika improvements kuhusu vifo vitokanavyo na dawa za usingizi na ngazi ni ndgo sana hili ni kwasababu wameboresha katika mitaala yao kwani sisi hili hatuwezi kulifanya jibu ni kwamba inawezekana ila Kuna kitu kilichofichwa ambayo hiki sio afya katika maboresho na utoaji huduma kwa watanzania zile ni afya za watu tupeni haki yetu ya kimasomo ili tuwe aproded hata leo huyu mtu anaesoma hii course awe proud na hata ikitokea kwenda kusoma nje aweze kwa mtaala huu wa sasa huyu mtu ataenda wapi kusoma nini kwasababu mtaala wetu mbovu nasio kwamba kwa bahati mbaya hili lipo chini ya uwezo wa serikali yetu tunaomba wizara iliangalie hili kama wizara ilileta hii course kuandaa wauguzi iseme na kama sivyo ituambie pia watu wanasoma lakn future zao hazionekani kabsa kwanini tunafikq huku? Katika tu hili pamoja naserikali kupambana kupunguza vifo vitokanavyo na hii idara sidhani kama vitapungua kwasababu hata wanasoma sahv hawako motivated kabsa na hawajui hata majukumu yao ni yapo huko makazi kwahiyo sioni kama hii changamoto na upungufu huu ukiisha,,,
    WANAFUNZI WALIOPO CHUO CHA AFYA MUHIMBILI WANAOSOMA SHAHADA YA USINGIZI NA GANZI SALAMA WAPEWE HAKI ZAO ZA KIMASOMO NA WATANZANIA KWA UJUMLA TUNAOMBA MABORESHO YA MTAALA WA ANAESTHESIA ILI MTANZANIA AKAHUDUMIWE KWAMAARIFA YALIYOJITOSHEREZA HATUTAKI KWENDA KUUA WATU KISA MTAALA TUPENI HAKI ZETU TUMEZUNGUKA HOFSI NYINGI TUMEKUWA TUKIAHIDIWA TUTAFANYIWA MABORESHO LAKINI IMEKUWA KAMA WIMBO MNATAKA TUKASABABISHE VIFO HUKO KISA MAARIFA HATUNA HII SIO HAKI HATA KITOGO
    HAKI YETU SISI HAIWAZUII WATU WENGINE KUPATA FURSA NA MAMBO MENGINE

Comments are closed.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV