Pato la Mtanzania laongezeka kwa Sh125,000

June 11, 2020 10:21 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya ulinganisho wa pato la Mtanzania kwa mwaka 2018 na mwaka 2019.
  • Kwa mwaka 2019, kila Mtanzania ameongeza wastani zaidi Sh125,000 katika pato lake.
  • Ongezeko la pato la Mtanzania linaenda sambamba na ongezeko la Pato la Taifa.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amesema pato la Mtanzania kwa mwaka limeongezeka kwa asilimia 5.1 kwa mwaka 2019 ikilinganishwa na lilivyokuwa mwaka 2018 ikiwa ni sawa ongezeko la zaidi ya Sh125,500.

“Mwaka 2019 pato la wastani la kila mtu lilikuwa Sh2.58 milioni (Sh2,577,967)  ikilinganishwa na Sh2.45 milioni (Sh2,452,406)  mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 5.1,” Dk Mpango amelieleza Bunge Alhamis (Juni11,2020) wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2019 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa mwaka 2020/21. 

Vilevile pato la wastani kwa kila mtu katika Dola za Marekani liliongezeka hadi kufikia dola za Marekani 1,121 mwaka 2019 kutoka Dola za Marekani 1,078 mwaka 2018.


Zinazohusiana


Sanjari na ongezeko la pato la kila Mtanzania Pato la Taifa pia lilikua kwa asilimia 7 ambayo ni sawa na ukuaji wa mwaka 2018.

Dk Mpango amesema sababu kubwa ni pamoja na uwekezaji katika miundombinu ya barabara reli na uwanja wa ndege, kuimarika kwa huduma za usafirishaji pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo. 

“Sekta zilizokuwa kwa viwango vikubwa kwa kipindi hicho ni pamoja na uchimbaji wa madini na mawe asilimia 17.7, ujenzi 14.8, sanaa na burudani (asilimia 11.2) na usafirishaji na uhifadhi wa mizigo kwa asilima 8.7,” amesema Dk Mpango.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV