NIDA yaanza kugawa vitambulisho vya Taifa Dar, Mbeya leo

December 13, 2023 7:21 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Zoezi hilo limeanza leo Disemba 12, 2023, litamalizika baada ya siku 14.
  • Wasiochangamkia fursa kuvifata wilayani

Dar es Salaam. Mamlaka ya Vitambulisho Tanzania (NIDA) imeanza  zoezi la kugawa vitambulisho ya Taifa kwa wakazi wa mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dar es Salaam na Mbeya.

Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano NIDA, Jumatatu, Disemba 11, 2023 inafanunua kuwa zoezi hilo lililoanza leo litafanyika ndani ya siku 14 katika ofisi za Serikali za mitaa, vitongoji na vijiji katika wilaya zote za  mikoa husika.

“Wananchi wote waliosajiliwa na kupatiwa Namba za Utambulisho wa Taifa (NINs) mnaombwa kujitokeza na kuchukua vitambulisho katika ofisi za Serikali za mitaa, ndani ya siku 14 tangu kuanza kugawiwa kwa vitambulisho hivyo ndani ya eneo husika,” imesema taarifa hiyo.

Aidha, NIDA imefafanua kuwa mwananchi atakayeshindwa kuchukua kitambulisho chake ndani ya muda uliopangwa katika eneo lake, atalazimika kukifuata Kitambulisho chake katika ofisi ya NIDA ya Wilaya anayoishi.

Huenda zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho vya Taifa likapunguza changamoto ya upatikanaji wa vitambulisho hivyo kwa baadhi ya watanzania walioshindwa kuvipata kwa wakati jambo lililokwamisha shughuli mbalimbali ikiwamo usajili wa namba za simu.

Itakumbukwa kuwa  Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, alitoa ahadi ya kumalizika kwa changamoto hiyo ifikapo mwezi Machi 2024 wakati akizungumza mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa ziarani mkoani Mtwara mwezi Septemba mwaka huu.


Soma zaidi:Punda wanavyorahisisha maisha ya wakazi Iziwa, Mbeya


Masauni aliongeza kuwa tayari Serikali imeshalipa fedha kwa mkandarasi anayetengeneza vitambulisho hivyo na kazi bado inaendelea.

“Katika bajeti iliyopita Serikali ilitenga Sh42.5 bilioni kwa ajili ya kutengeneza kadi milioni11, fedha hizi zimeshalipwa kwa mkandarasi na anaendelea kuzitengeza,” alifafanua Masauni Septemba 16, 2023.

Kwa mujibu wa NIDA, mpaka kufikia Oktoba 31 mwaka huu watu milioni  24.2 wamesajiliwa, kati ya hao milioni 20.5 tayari wameshapatiwa namba za utambulisho (NINs) zinazotumiwa katika shughuli mbalimbali.

Kwa upande wa Vitambulisho vya Taifa hadi kufikia Oktoba, 2023, NIDA imezalisha vitambulisho milioni 16.2 kati ya hivyo milioni 13.9 vimesambazwa kwa wananchi nchi nzima.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV