NIDA kubadili bure vitambulisho vinavyofutika maandishi

November 27, 2025 6:21 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma kupitia vitambulisho hivyo bila usumbufu.

Dar es Salaam. Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza kubadilisha bure vitambulisho vya taifa vilivyofutika maandishi ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma kupitia vitambulisho hivyo bila usumbufu.

Akizungumza leo Novemba 27, 2025, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, amesema wananchi wote wenye vitambulisho vilivyoanza kufifia maandishi wanapaswa kuvirejesha katika Ofisi za NIDA za wilaya ambapo watapatiwa vitambulisho vipya bila malipo.

Kaji amesema hatua hiyo inalenga kutatua changamoto iliyolalamikiwa na baadhi ya wananchi, ambao wengine wameshindwa kuvitumia vitambulisho vyao kutokana na vitambulisho hivyo kutosomeka kwa kufifia maandishi. 

“Tumekuja na suluhu ya vitambulisho vinavyofutika maandishi. Kama unacho, ukirudishe katika ofisi ya wilaya, unaandika jina na unasaini, na utapata kitambulisho kipya bila malipo,” amesema Kaji.

Hata hivyo, amesisitiza kuwa utaratibu huo unawahusu tu wale ambao vitambulisho vyao vimeharibika kutokana na hitilafu ya kiufundi, na si kutokana na uzembe au uharibifu wa makusudi akisisitiza kuwa walioharibu vitambulisho hivyo kwa bahati mbaya au makusudi watalazimika kulipia gharama.

Wananchi wote wenye vitambulisho vilivyoanza kufifia maandishi wanapaswa kuvirejesha katika Ofisi za NIDA za wilaya ambapo watapatiwa vitambulisho vipya bila malipo. Picha | Diramakini

“Kuna wale walioviharibu mfano mtu alikalia kikavunjika, hao watalazimika kulipia gharama ya Sh 20,000 ya kutengeneza kitambulisho kipya,” amefafanua Kaji.

Aidha, Kaji amesema vitambulisho vya awali vilivyokuwa na ukomo wa muda havitakuwa tena na kikomo hicho huku akifafanua kuwa, kwa yeyote anayekereka na tarehe hiyo kuendelea kuonekana kwenye kitambulisho chake, atalazimika kulipia gharama ili kubadilishiwa kitambulisho kipya.

NIDA imetoa wito kwa wananchi kufika katika ofisi zao za wilaya kwa wakati, ili kuhakikisha wanapata vitambulisho sahihi na vyenye ubora unaotakiwa.

2 thoughts on “NIDA kubadili bure vitambulisho vinavyofutika maandishi

  1. Mim namba yangu ya nida haitumiki nikiingiza namba mda wa kuweka alama za vidole inasumbua na nipo mbali na uduma mnanisaidiaje

    1. Habari Stephen Masaga, pole sana kwa changamoto.
      Jaribu kutembelea ofisi za NIDA zilizo karibu nawe, au ofisi ya Halmashauri uliyoombea kitambulisho chako utaweza kusaidiwa. Karibu sana na usiache kutufuatilia Nukta Habari.

Comments are closed.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV