Mvua za masika: Fursa, tishio kwa wafugaji wa samaki Tanzania

February 18, 2020 3:12 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • TMA yawataka kuchukua tahadhari ya ujio wa mvua za masika na kuimarisha miundombinu ya mabwawa. 
  • Wataalam washauri njia za mbadala za kuimarisha mabwawa ya samaki.
  • Serikali yawaomba wawekezaji kuanzisha viwanda vya kutengeneza vyakula vya samaki. 

Dar es Salaam. Vijana waliowekeza na wanaotaka kuwekeza katika ufugaji wa samaki Tanzania wametakiwa kuchukua tahadhari na kutumia vizuri ujio wa mvua za masika kuongeza uzalishaji utakaowasaidia kuongeza fursa za ajira na kipato cha kuendesha maisha yao.

Samaki hao ni pamoja sato na kambale wanaofugwa kwenye mabwawa ya asili na ya kutengenezwa. Samaki hao hutumika katika shughuli za biashara, maonyesho, utalii na chakula cha kwa ajili ya watu.

Maji yanayotumika katika mabwawa hayo hutoka katika vyanzo mbalimbali ikiwemo mito, maziwa, bahari na mvua za msimu za masika zinazotarajiwa kuanza Machi mwaka huu.  

Kwa mujibu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, mabwawa ya samaki yamezidi kuongezeka nchini hadi 26,445 katika mwaka wa fedha wa 2018/2019 kutoka mabwawa 24,302 mwaka 2017/2018. Mabwawa hayo mwaka wa fedha wa 2018/19 yalichangia uzalishaji wa samaki tani 30,000 waliokuwepo kwenye maji madogo yaani maziwa madogo ya kati, mito na mabwawa.

Hata wakati vijana wakichangamkia fursa hizo za ufugaji wa samaki wametakiwa kufuatilia kwa taarifa za hali ya hewa zinazohusu mvua za msimu ili kuepuka kupata hasara na kupoteza miundombinu ya ufugaji.  


Zinazohusiana


TMA yawatahadharisha

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wafugaji wa samaki kujiandaa vema na ujio wa mvua za masika  zitakazoanza mwezi Machi hadi Mei, 2020  ili kuhakikisha wanaendelea kufaidika na shughuli hiyo yenye mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi binafsi na Taifa.

Kwa mujibu wa TMA, mvua hizo zinatarajiwa kunyesha katika mikoa inayopata vipindi viwili vya mvua kwa mwaka ikiwemo mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, Dar es Salaam, Pwani ikijumuisha kisiwa cha Mafia, Tanga na maeneo ya kaskazini mwa mkoa wa Morogoro pamoja na  visiwa vya Unguja na Pemba.

Mikoa mingine ni Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

TMA imewataka wavuvi kuchukua tahadhari ya kuimarisha miundombinu ya mabwawa yao kwasababu maji yataongezeka na inawezekana yakatatiza shughuli za uzalishaji wa samaki na kuwakosesha soko la bidha hiyo.

 “Sekta ya uvuvi inaweza pia kuathirika kutokana na uwezekano wa ongezeko kubwa la maji katika mabwawa ya kufugia samaki, hivyo wafugaji wa samaki wanashauriwa kuimarisha miundombinu ya mabwawa yao,” anasema Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi na kuongeza kuwa hiyo inatokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa na jinsi inavyotarajiwa kuwa kwa kipindi chote cha msimu.

Uimarishaji wa miundombinu ni pamoja kingo za mabwawa, mifereji ya kuingizia maji na kutolea maji ili kuhakikisha mabwawa yanapata maji yanayohitajika kwa wakati husika. 

Dk Kijazi anasema mvua hizo za masika zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya mkoa iliyotajwa, isipokuwa kwa maeneo ya mkoa wa Kagera, magharibi mwa mkoa wa Geita, kaskazini mwa mkoa wa Kigoma, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia) pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani.

Hiyo inamaanisha mvua zitakuwa nyingi kuwawezesha wavuvi kupata maji ya kutosha kwa ajili ya ufugaji wa samaki lakini wanatakiwa pia kuchukua tahadhari ya vipindi vifupi vya mvua kubwa ili kuepuka madhara zaidi. 

Hata katika maeneo ambayo hayatapata mvua za kutosha, bado TMA inawashauri wavuvi kuvuna maji na kuyahifadhi ili kuhakikisha wanakuwa na maji ya kutosha ili kuwawezesha samaki kuendelea kuishi. 

Hata wakati vijana wakichangamkia fursa hizo za ufugaji wa samaki wametakiwa kufuatilia kwa taarifa za hali ya hewa zinazohusu mvua za msimu ili kuepuka kupata hasara na kupoteza miundombinu ya ufugaji. Picha|Mtandao. 

Katika hatua nyingine, TMA imewataka watumiaji wa taarifa za hali ya hewa ikiwa ni pamoja wafugaji wa samaki kuendelea kutafuta, kupata na kufuata ushauri wa wataalam katika sekta husika.

Mtaalam wa samaki kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Christopher Sway ameiambia Nukta (www.nukta.co.tz) kuwa ili mabwawa ya samaki yasivunjike katika kipindi cha mvua nyingi,  wafugaji wanatakiwa kuyaelewa mazingira waliyopo na kuhakikisha mikondo inayoingiza maji kwenye bwawa iko vizuri na inapitisha maji kwa kiasi kinachotakiwa.

Anasema kama maji ni mengi, mfugaji anatakiwa kuchepusha maji yasiingie kwenye bwawa na kuyaelekeza maeneo mengine kuepusha kingo za bwawa kufunjika. 

“Kingo za bwawa zinatakiwa ziwe zimechongwa kuegemea nje ili kukinga bwawa lisibomoke na kukusaidia uweze kuingia bwawani kwa urahisi tofauti na kingo zikiwa zimesimama. Ni vema bwawa likawekewa mabomba pembeni ya kutolea maji ili kuhakikisha maji yanayoingia hayavuki kingo zake,” anasema Sway. 


Serikali yabainisha mikakati ya kuinua ufugaji wa samaki

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema licha ya Tanzania kuwa na maeneo mazuri kwa ajili ya ufugaji wa samaki lakini bado Taifa alifaidiki vya kutosha na sekta hiyo ndogo ya uvuvi kutokana na changamoto za teknolojia.

Ulega amewaomba wawekezaji kuwekeza katika teknolojia na viwanda vya kutengeneza vyakula vya samaki ili kuwafungulia fursa zaidi vijana kufaidika na ufugaji wa samaki katika maeneo yao. 

“Nawahimiza wadau wa sekta binafsi kuingia katika uzalishaji wa samaki na wengine kutengeneza chakula cha samaki,” alisema Ulega wakati wa uzinduzi wa shamba la kufugia samaki la  Righa’s Safina’s BigFish la jijini Dar es Salaam Februari 13, 2020,

Naye Balozi wa Netherland nchini Tanzania, Jeroen Verheul akizungumza katika uzinduzi huo amesema Serikali ya Tanzania ifanikiwe katika kuboresha ufugaji wa samaki inatakiwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuondoa kodi katika malighafi za uvuvi zinazoingia nchini ili kuwawezesha wawekezaji kutumia teknolojia rahisi ya ufugaji.

Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018 kinaeleza kuwa mauzo ya samaki na mazao yake nje ya nchi yamepungua kwa mwaka 2018 hadi dola za Marekani milioni 158.4 (Sh365.5 bilioni ) kutoka dola milioni 193 (Sh445.6 bilioni) mwaka 2017 sawa na upungufu wa asilimia 17.9 ndani ya mwaka mmoja.  

“Upungufu huo ulitokana na kushuka kwa kiasi cha samaki na mazao ya samaki kilichouzwa nje,” inasomeka sehemu ya kitabu hicho.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV