Mjadala bei taa za umemejua waibuka, wavuvi wakisubiri tamko la Serikali

January 13, 2023 5:18 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Wadai makampuni yanapendekeza kupandisha bei ambayo hawawezi kuimudu.
  • Wasubiri Serikali itoe tamko kama waendelee kutumia taa hizo au la.

Mwanza. Baadhi ya wavuvi mkoani Mwanza wamesema mpaka sasa hawajapata mrejesho wa taa za umemejua kama wanapaswa kuendelea kuzitumia katika shughuli zao baada ya kuhusishwa na uvuvi haramu. 

Sintofahamu hiyo ya wavuvi imekuja ikiwa ni takriban miezi miwili tangu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki kuagiza makampuni kuzifanyia tathmini taa hizo kama zinafaa kuendelea kutumika na wavuvi.

Alitoa agizo hilo kwenye mkutano uliokutanisha viongozi wa Serikari na wadau wa sekta ya uvuvi kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa Novemba 17, 2022 na kueleza kuwa tafiti za awali zimebainisha kuwa taa za umemejua zenye mwanga mkali zinachangia katika masuala ya uvuvi haramu.

Kutokana na changamoto hiyo, Waziri Ndaki alitoa miezi miwili hadi Januari 1, 2023 kwa kampuni zinazotengeneza taa hizo kuhakikisha zinafanyia majaribio taa zake kama zinafaa kwenye uvuvi.

“Tunatoa miezi miwili baada ya mapumziko ya sherehe za mwaka mpya tutakuja na mrejesho hapa kama taa hizo zinafaa kuvulia au lah! Vinginevyo, tutarudi kwenye matumizi ya kalabai na taa za chemli,” alisema Ndaki. 


Zinazohusiana:


Hata hivyo, baadhi ya wavuvi wamesema mpaka sasa hawajaona wataalam hao visiwani kwenda kufanyia majaribia taa hizo.

“Tunaendelea kutumia taa za umemejua, mpaka sasa hatujaambiwa lolote na sisi tunaendelea kuzitumia kuvua samaki mpaka tutakapoambiwa vinginevyo,” amesema Masabo John, mvuvi wa jijini Mwanza. 

Akizungumza na Nukta habari (www.nukta.co.tz) kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa wavuvi wilaya ya Sengerema, Hassan Gembale amesema bado wanasubiri maelekezo ya Waziri kuhusu matumizi ya taa hizo ingawa changamoto ipo kwenye bei.

“Changamoto ipo kwenye bei kwa maana taa tunazotumia tunanunua kati ya Sh30,000 hadi 100,000 hali inayosababisha baadhi ya wavuvu kutumia taa nyingi kwenye mtego mmoja ambazo zinachangia uvuvi haramu,” amesema Gembale.

Amesema mapendekezo ya makampuni yaliyoruhusiwa na Waziri ni kuuza taa hizo kuanzia Sh500,000 hadi milioni 1, kiwango ambacho baadhi ya wavuvi wanasema ni kikubwa na hawawezi kukimudu.

“Kwa hiyo tulimuomba Waziri hayo makampuni yapunguze bei ya taa hizo ili kila mvuvi amudu kununua lakini mpaka muda alioutoa waziri hakuna taarifa zozote hivyo wavuvi wanaendelea kutumia taa zile zile za awali,” amesema Gembale.

Ujio wa umemejua ambazo ni rafiki wa mazingira umesaidia wavuvi wa kupata mwanga wa uhakika wakiwa ziwani kuvua samaki na dagaa bila hofu ya kukosa nishati hiyo muhimu.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV