Rais Samia kugawa vifaa vya kisasa vya uvuvi ziarani mkoani mwanza

January 26, 2024 12:11 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Atawasili Januari 29 na kuanza ziara yake asubuhi ya Januari 30 mwaka huu.
  • Wavuvi watakao nufaika ni kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Geita na Simiyu.

Mwanza. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku moja jijini Mwanza kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kisasa kwa wavuvi wa mikoa mitano ya kanda ya ziwa.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla, aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo leo Januari 26, 2024 amesema Rais Samia atawasili Januari 29 na kuanza ziara yake asubuhi ya Januari 30 mwaka huu.

“Januari 30,2024 asubuhi atakabidhi vifaa vya uvuvi kwa vikundi mbalimbali vya wavuvi vilivyopo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, hafla itakayofanyika katika Uwanja wa Nyamagana,” amesema Makalla.


Soma zaidi:Ufahamu mwenendo wa ufaulu matokeo kidato cha nne kwa miaka mitano Tanzania


Makalla amebainisha kuwa vikundi vitakavyonufaika na zana hizo za kisasa ni vile vilivyosajiliwa na kufanya shughuli za uvuvi katika mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera, Geita na Simiyu.

Baada ya kukabidhi vifaa hivyo Rais Samia atazungumza na wavuvi na wananchi wa mkoa huo na maeneo jirani.

“Rai yangu kwa wananchi wajitokeze kumlaki atakapowasili katika uwanja wa ndege pia waje kumsikiliza katika mkutano wake baada ya kukabidhi vifaa vya uvuvi,” amesema Makalla.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla (kulia) akisistiza jambo katika mkutano na wanahabari jijini Mwanza Januai 26, 2024.Picha|Mariam John.

Vifaa vya kisasa kukuza sekta ya  uvuvi

Makalla amesema zana hizo zilizotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi zitawasaidia wavuvi kuondokana na changamoto ya matumizi ya zana duni za uvuvi wa samaki zilizopitwa na wakati.

Zoezi hilo la kukabidhi vifaa vya kisasa kwa wavuvi ni muendelezo wa jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta hiyo inayochangia katika ukuaji wa pato la Taifa.

Itakumbukwa kuwa Agosti, 2023 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega aliyekuwa akizungumza na vijana waliopata mafunzo ya ufugaji samaki katika vizimba alisema Serikali itawakopesha wavuvi nchini kote boti za kisasa zaidi ya 150 ili waweze kuboresha shughuli zao na kuongeza uzalishaji wa samaki.

Mbali na ahadi hiyo Ulega alisema ili kuboresha sekta hiyo Rais Samia atatoa Sh20 bilioni zitakazosaidia miradi mbalimbali ya uvuvi ikiwemo ya ufugaji samaki katika vizimba.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

NMB BANK YATANGAZA GAWIO LA SH610 KWA HISA 2025

Nukta TV

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

🔴LIVE: ULEGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA UJENZI BUNGENI

Nukta TV