Miradi 9 itakayobadilisha sura ya mawasiliano, habari Tanzania

May 19, 2023 10:20 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni ujenzi wa mkongo wa Taifa na kituo cha Tehama.

  • Pia Serikali itaendeleza mradi wa anwani za makazi. 

Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeomba kuidhinishiwa Sh212.5 bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2023/24 huku ikipanga kutekeleza miradi tisa ikiwemo mkongo wa Taifa kuimarisha sekta ya mawasiliano na habari nchini. 

Kati ya fedha hizo, Sh30.5 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambapo Sh18.5 bilioni ni kwa ajili ya mishahara na Sh11.9 bilioni ni za  matumizi mengineyo.

“Kiasi cha Sh181.9 bilioni ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo Sh146.7 bilioni ni fedha za ndani na Sh35.2 bilioni ni fedha za nje,” amesema Waziri wa wizara hiyo, Nape Nnauye leo Mei 19, 2023 Bungeni jijini Dodoma. 

Hata hivyo, bajeti hiyo imeshuka kutoka Sh282.1 bilioni ya mwaka 2022/23 ambapo hadi kufikia Aprili 30 mwaka huu, wizara hiyo ilikuwa imepokea na kutumia Sh125.1 bilioni. 

Miradi itakayotekelezwa

Ili kuhakikisha Serikali inaharakisha kuwa na jamii yenye habari sahihi na iliyowezeshwa kidigitali kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii, wizara inakusudia kutekeleza miradi tisa mwaka ujao wa fedha.

Waziri Nape amesema katika mwaka ujao wa fedha watatumia Sh80 bilioni kutekeleza kazi ya ujenzi wa mkongo wa Taifa wa mawasiliano kukamilisha ujenzi wa kilomita 1,600 za mkongo na vituo vipya 15 vya kutolea huduma za mkongo ili kuongeza wigo wa utoaji wa huduma hadi ngazi za wilaya nchini. 

 Kuimarisha uwezo wa taasisi katika utekelezaji wa majukumu

“Mradi huu umelenga kuboresha na kuimarisha uwezo wa watalaam ndani ya wizara katika matumizi ya Tehama katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku, kutoa elimu kwa wananchi kutambua uchumi wa kidijitali unaowezeshwa na matumizi ya Tehama pamoja na matumizi sahihi na salama ya Tehama yanayozingatia sheria, taratibu na kanuni,” amesema Nape. 

Katika Mwaka wa Fedha 2023/24 Sh4.5 bilioni fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu.

Wizara hiyo inakusudia kutumia Sh24 bilioni katika mradi wa anuani za makazi ambapo baadhi ya shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na kuhakiki taarifa zilizokusanywa wakati wa Operesheni Anwani za Makazi katika Halmashauri 80 na kuratibu uwekaji wa miundombinu yake.

Ujenzi wa kituo kikuu na vituo vidogo vya kuendeleza ubunifu katika Tehama

Mradi huu unalenga kuimarisha na kuendeleza ujuzi kwa wabunifu katika masuala ya Tehama nchini kwa lengo la kukuza vipaji na kuongeza wigo wa vijana kujiajiri katika shughuli mbalimbali. 

Kwa mwaka 2023/24 Sh8.5 bilioni zitatumika kusimamia ujenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Kuendeleza Watalaam, Tafiti na Ubunifu wa Tehama jijini Dodoma na Chuo cha Tehama Kigoma, kuanzisha vituo atamizi vya Tehama katika vyuo vikuu vya umma na maeneo maalum ya kiuchumi kote nchini.

Mradi mwingine wa Tanzania ya Kidijitali unaolenga kuleta mabadiliko ya kidijitali kwa kuwezesha maunganisho ya kijiditali ya kikanda na kimataifa na kukuza uchumi wa kidijitali. 

Matokeo ya mradi huu ni pamoja na kuongeza na kubuni ajira zitakazotokana na ubunifu wa Tehama, ukuzaji wa viwanda vidogo vidogo (SMEs na SMMEs); kukuza ustadi wa wataalamu wa ndani na nje ya Serikali  na kuongeza uwezo wa utoaji wa Huduma za Serikali kwa kuwezesha uwepo wa intaneti bora ya bei nafuu na ya uhakika kwa ajili ya matumizi ya Serikali ili kumnufaisha mwananchi. 

Sh35.2 bilioni zimetengwa kutekeleza mradi huu.

“Katika mwaka wa fedha 2023/24 Wizara inakadiria kutumia Sh3.3 bilioni fedha za ndani kwa ajili ya kutekeleza mradi wa kuendeleza ubunifu na utengenezaji wa vifaa vya Tehama,” amesema Nape wakati akianisha mradi wa sita.

Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na  ujenzi wa vituo vitatu vya kanda vya watengenezaji wa bidhaa za Tehama, kuendelea na ujenzi wa kituo cha kuwezesha uanzishwaji wa kampuni changa za Tehama cha Dar es Salaam na kutengeneza mfumo jumuishi utakaounganisha usajili na uendelezaji wa wataalam na wabunifu wa Tehama.

Mradi wa saba utakuwa ni upanuzi wa usikivu kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) unaolenga kuboresha upanuzi wa usikivu wa shirika nchi nzima. Kwa mwaka wa fedha 2023/24 wizara inakadiria kutumia Sh15 bilioni kufanikisha mradi huo.

Mradi wa kufunga mtambo mpya wa kisasa wa uchapaji

Mradi huu unalenga kuwezesha kampuni ya Magazeti Tanzania (TSN) kufunga mtambo mpya wa kisasa wa uchapaji. 

Katika mwaka wa fedha 2023/24, Sh10 bilioni zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza shughuli zifuatazo: ukamilisha ujenzi wa kiwanda cha uchapaji; kukamilisha ufungaji wa mitambo ya kisasa ya uchapaji; na ununuzi wa vitendea kazi ikiwemo magari kwa ajili ya kuongeza uzalishaji.

Mradi wa mwisho ni wa habari kwa umma. Mradi huu unalenga kukusanya, kuchakata, kuandaa na kusambaza habari na taarifa kwa wananchi kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Serikali ikiwemo Sera, Sheria, Mikakati, Programu na Miradi zinazotekelezwa na Serikali. 

Vilevile, mradi unakusanya taarifa za mrejesho kutoka kwa wananchi kwa lengo la kupata maoni ya wananchi katika utekelezaji wa majukumu. Utatumia Sh1.5 bilioni.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV