Mfumuko wa bei za bidhaa, huduma muhimu washuka Februari

March 9, 2023 12:00 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Umeshuka hadi asilimia 4.8 kutoka asilimia 4.9 ya mwaka ulioishia Januari 2023.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania umeshuka hadi kufikia asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia Februari 2023 kutoka asilimia 4.9 iliyorekodiwa Januari mwaka huu.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

“Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Februari, 2023 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023,” imeeleza taarifa ya NBS iliyotolewa leo Machi 9, 2023.

Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia Februari, 2023 umepungua hadi asilimia 9.6 kutoka asilimia 9.9 kwa mwaka ulioishia Januari, 2023. 

“Kwa upande mwingine, mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Februari, 2023 umepungua pia hadi asilimia 2.8 kutoka asilimia 3.0 ilivyokuwa mwezi Januari, 2023,” imeeleza NBS.

Kwa mujibu wa ofisi hiyo, mfumuko wa bei umekuwa na mwenendo imara ambao uko kati ya asilimia 3.6 na asilimia 4.9. 

NBS imeeleza kuwa fahirisi za bei za Taifa kati ya Januari 2023 na Februari 2023 zimeongezeka kwa asilimia 0.4. 

Kuongezeka kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula. 

Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa hahirisi za bei ni pamoja na ngano kwa asilimia 1.2, mtama (asimimia 0.7), ulezi (asilimia 3.3), unga wa ngano (asilimia 1.2), unga wa mtama (asilimia 1.9) na unga wa mahindi kwa asilimia 2.4.

Samaki wabichi kwa asilimia 0.4, dagaa wakavu (asilimia 0.7), matunda (asilimia 0.6), karanga mbichi (asilimia 4.4), mbogamboga (asilimia 1.7), viazi vitamu (asilimia 6.7), mihogo mibichi (asilimia 4.0) na maghimbi kwa asilimia 1.4.

Bidhaa zingine za vyakula ambazo bei zake zimepanda ni maharagwe kwa asilimia asilimia 2.8,  choroko kavu (asilimia 0.8), njegere kavu (asilimia 1.0), kunde kavu (asilimia 1.0), unga wa muhogo (asilimia 5.6) na vinywaji visivyo na kilevi kwa asilimia 0.7.

Kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kuongezeka kwa fahirisi za bei ni pamoja na  nguo za wanawake kwa asilimia 0.3, sare za shule (asilimia 0.4), viatu vya wanaume (asilimia 0.5), kuni (asilimia 2.3), mkaa (asilimia 1.6), karo za shule (asilimia 0.4) na huduma ya malazi kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni kwa asilimia 2.1. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Rais Samia: AFCON ni fursa, wawekezaji karibuni kuwekeza

Nukta TV

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Utani wa Rais Samia, matokeo kati ya Simba na Yanga

Nukta TV

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Rais Samia awataka wananchi wa Kizimkazi kutunza miundombinu ya maji

Nukta TV