Mfumuko wa bei washuka kwa mara ya pili Tanzania

April 11, 2023 1:17 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Umeshuka hadi kufikia asilimia 4.7 kwa mwaka ulioishia Machi 2023 kutoka asilimia 4.8 iliyorekodiwa Februari mwaka huu.
  • Umechagizwa zaidi na kupungua kwa gharama za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania imeendelea kushuka kwa miezi miwili mfululizo hadi kufikia asilimia 4.7 kwa mwaka ulioishia Machi 2023 ikichagizwa zaidi na kupungua kwa gharama za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula.

Mfumuko wa bei wa Taifa hupima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Mfumuko wa bei wa Machi umeshuka kutoka asilimia 3.8 iliyorekodiwa Februari mwaka huu ambapo pia ulishuka kutoka asilimia 3.9 ya mwaka ulioishia Januari 2023. 

Taarifa ya mfumuko wa bei ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyotolewa leo Aprili 11, 2023 imeeleza kuwa kushuka kwa mfumuko wa bei kumechangiwa na kupungua kwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na zisizokuwa za chakula ikilinganishwa na Februari mwaka huu. 


Zinazohusiana:


Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Machi 2023 ni mchele kutoka asilimia 32.7 hadi asilimia 32, unga wa ngano (kutoka asilimia 18.8 hadi asilimia 16.1), unga wa mtama (kutoka asilimia 5.8 hadi asilimia 5.6) na matunda kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 7.4.

Viazi vitamu mfumuko wake umeshuka kutoka asilimia 12.5 hadi asilimia 7.8, mihogo mibichi (kutoka asilimia 23.3 hadi asilimia 20.9), choroko (kutoka asilimia 7.9 hadi asilimia 5.2), njegere kavu (kutoka asilimia 4 hadi asilimia 2.2) na kunde kavu kutoka asilimia 16.2 hadi asilimia 12.9.

Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua kwa mfumuko wa bei ni nguo za wanaume kutoka asilimia 2.2 hadi asilimia 1.6, nguo za wanawake (kutoka asilimia 2.9 hadi asilimia 2.8),  viatu vya wanaume (kutoka asilimia 2.6 hadi asilimia 2.3) na viatu vya watoto kutoka asilimia 2.7 hadi asilimia 2.6.

Pia mfumuko wa bei za bidhaa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba zimeshuka kutoka asilimia 5 hadi asilimia 4, gesi (kutoka asilimia 9.1 hadi asilimia 9), kuni (kutoka asilimia 13 hadi asilimia 8.2), mazulia (kutoka asilimia 1.5 hadi asilimia 1.1) na dizeli kutoka asilimia 27.8 hadi asilimia 23.2.

Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia Machi 2023 umeongezeka kidogo hadi asilimia 9.7 kutoka asilimia 9.6 kwa mwaka ulioishia Februari 2023. 

“Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Machi 2023 umepungua kidogo hadi asilimia 2.7 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Februari 2023,” imeeleza taarifa ya NBS. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV