Mfumuko wa bei za bidhaa, huduma wapaa Tanzania

February 9, 2023 1:56 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  •  Umeongezeka hadi asilimia 4.9 mwaka ulioishia Januari 2023 kutoka asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia Disemba 2022. 

Dar es Salaam. Kasi ya mfumuko wa bei muhimu za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Januari 2023 umeongezeka hadi asilimia 4.9 kutoka asilimia 4.8 kwa mwaka ulioishia Disemba 2022. 

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) katika taarifa yake iliyotolewa leo Februari 9, 2023 imesema kuongezeka kwa mfumuko kwa mwaka ulioishia Januari 2023 kumechangiwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

Baadhi ya bidhaa za vyakula ambazo mfumuko wake wa bei umeongezeka ni ngano kutoka asilimia 6 hadi asilimia 7.7, unga wa mtama (kutoka asilimia 1 hadi asilimia 3.9), samaki (kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 4.3) na matunda kutoka asilimia 1.9 hadi asilimia 5.5.

Bei ya mbogamboga imeongezeka kutoka asilimia 3.6 hadi asilimia 5.2, viazi vitamu (kutoka asilimia 3.9 hadi asilimia 5.3),  choroko (kutoka asilimia 1.3 hadi asilimia 5.6) na kunde kutoka asilimia 8.7 hadi asilimia 13.9.


Zinazohusiana


Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonyesha kuongezeka kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Januari 2023 ikilinganishwa na mwaka ulioishia Disemba 2022 ni pamoja na nguo za wanawake kutoka asilimia 2.6 hadi asilimia 2.7, viatu vya wanawake (kutoka asilimia 3.4 hadi asilimia 3.5) na vifaa muhimu kwa matumizi ya nyumbani kutoka asilimia 2.2 hadi asilimia 3.5.

Dizeli imeongezeka kutoka asilimia 27.4 hadi asilimia 33.1, petroli (kutoka asilimia 3.7 hadi asilimia 4.7), ada za shule (kutoka asilimia 0.7 hadi asilimia 2.9) na huduma ya malazi kwenye hoteli na nyumba za kulala wageni kutoka asilimia 0.9 hadi asilimia 3.8.

“Mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Januari 2023 umeongezeka hadi asilimia 9.9 kutoka asilimia 9.7 kwa mwaka ulioishia Disemba 2022,” imeeleza NBS katika taarifa hiyo.

Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa  umeongezeka kidogo hadi asilimia 3 kutoka asilimia 2.9.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV