Matokeo kidato cha nne 2021 hadharani
- Asilimia 87.3 ya watahiniwa wamefaulu mtihani huo.
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha nne uliofanyika mwaka 2021 huku asilimia 87.3 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo wakifaulu.
Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amewaeleza wanahabari leo Januari 15, 2022 jijini Dar es Salaam kuwa watahiniwa wa shule 422,388 sawa na 87.3 kati ya watahiniwa 483,820 wenye matokeo ya kidato cha nne wamefaulu mitihani yao muhimu kuingia katika elimu ya kidato cha tano.
“Ufaulu wa watahiniwa umeongezeka kwa asilimia 1.46 ikilinganishwa na mwaka wa 2020,” amesema Dk Msonde.
Kupata matokeo ya kidato cha nne mwaka 2021 bonyeza hapa
Aidha, Dk Msonde amesema ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa umechunguzwa na kubainishwa kuwa jumla ya watahiniwa waliofaulu vizuri yaani daraja la I hadi la III wako 173, 422 sawa na asilimia 35.8 wakiwemo wasichana 75,056.
“Mwaka 2020 watahiniwa waliopata madaraja ya juu ya daraja la I, II na la III walikuwa 152,909 sawa na asilimia 35.1 hivyo ubora wa ufaulu wa matokeo haya kidato cha nne 2021 umeongezeka kwa asilimia 0.74,” amesema Dk Msonde.
Latest



