Matokeo darasa la saba yatangazwa, ufaulu ukiongezeka kwa asilimia 1.2

November 21, 2020 12:29 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Umeongezeka kutoka asilimia 81.5 mwaka 2019 hadi asilimia 82.68 mwaka huu.
  • Jumla ya watahiniwa 833,672 kati ya milioni 1.01 waliotunukiwa matokeo wamefaulu.
  • Wanafunzi 14,364 hawakufanya mitihani kutokana sababu mbalimbali ikiwemo utoro.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2020 huku ufaulu ukiongezeka kidogo kwa asilimia 1.18. 

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde aliyekua akitangaza matokeo hayo leo Novemba 21, 2020 Jijini Dar es Salaam amesema watahiniwa 833,672 kati ya milioni 1.01 wamefaulu ikiwa ni sawa na asilimia 82.68.

Ufaulu huo wa mwaka huu upo juu kidogo ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2019 wa asilimia 81.5.

Dk Msonde amesema kati ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo wa elimu ya msingi ni 430,755 ambao ni sawa na asilimia 82.24 na wavulana ni 402,917 sawa na asilimia 83.15. Wanafunzi waliofaulu ni wale waliopata alama 100 na zaidi kati ya alama 250.

Katika mtihani huo watahiniwa milioni 1.02 walisajiliwa kufanya mtihani huo uliofanyika Oktoba mwaka huu wakiwemo wasichana 530,692 sawa na asilimia 51.83.


Soma zaidi: 


Dk Msonde amesema watahiniwa milioni 1.01 sawa na asilimia 98.50 ya waliosajiliwa walifanya mtihani huo. Kati yao wasichana walikuwa 524,456.

“Watahiniwa 14,364 sawa na asilimia 1.4 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro na ugonjwa,” amesema Dk Msonde.

Elimu ya msingi ni kiungo muhimu kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo ya sekondari hadi elimu ya juu Tanzania.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV