Majaliwa awatega wamachinga mitaji kuendesha biashara

May 24, 2022 1:43 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa akizungumza leo Mei 24, 2022 wakati  akikagua masoko ya Mbauda, Machame, na Kilombero yaliyopo jijini Arusha amesisitiza suala la wamachinga hao kufanya biashara kwenye masoko wapate huduma stahiki. Picha | Ofisi ya Waziri Mkuu.


  • Awataka wafanye biashara katika maeneo yanayotambulika.
  • Hiyo itakuwa rahisi kuwatambua na kuwapa mikopo.

Arusha. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga wahakikishe kuwa wanafanya biashara kwenye maeneo yanayotambulika ili waweze kupatikana kwa urahisi na waweze kupata mikopo ya mitaji.

Kauli ya Majaliwa ni mwendelezo wa Serikali kuwapanga na kuwawekea mzuri ya kufanyia biashara wamachinga, zoezi ambalo lililoasisiwa na Rais Samia Suluhu Hassan Oktoba 2021.

Majaliwa aliyekuwa akizungumza leo Mei 24, 2022 wakati  akikagua masoko ya Mbauda, Machame, na Kilombero yaliyopo jijini Arusha amesisitiza suala la wamachinga hao kufanya biashara kwenye masoko wapate huduma stahiki. 

“Niwasihi ndugu zangu wafanyabiashara, fanyeni biashara zenu kwenye meza zinazojengwa kwenye haya masoko. Hiyo meza hapo sokoni ndiyo anuani yako. Uongozi wa soko utajua uko wapi, unauza nini, vina thamani gani. Pia utakudhamini kwa sababu unajulikana unafanyia wapi biashara yako,” amesema Majaliwa.


Zinazohusiana:


Majaliwa amewasisitiza wamachinga kuwa wakiwa sokoni watapata fursa muhimu kama kupata mikopo ili kukuza mitaji yao na hatimaye kuwa wafanyabiashara wakubwa. 

“Suala la mitaji, Mheshimiwa Rais Samia alishakutana na wakuu wa mabenki nchini na kuwaomba waweke vigezo ambavyo vitasaidia wajasiriamali wadogo kukopesheka. 

“Ili ukopesheke, ni lazima uwe na anuani, ukiwa na anuani ni rahisi kufuatiliwa unaendeleaje na biashara yako,  mtaji wako ni kiasi gani na pia kupima uwezo wako wa kurejesha endapo utapata huo mkopo,” amesema Majaliwa.

 

Changamoto za masoko waliyohamishiwa wamachinga

Waziri Majaliwa amekagua ujenzi wa masoko matatu jijini Arusha (Mbauda, Machame, na Kilombero) na kubaini mapungufu kadhaa ikiwemo ukosefu wa maji, umeme, uhaba wa vyoo na bugudha za askari mgambo.

Masoko hayo ni miongoni mwa maeneo mbalimbali waliyohamishiwa wamachinga lakini bado yanakabiliwa na changamoto mbalimbali za miundombinu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV