Magufuli azungumzia chanjo, maambukizi ya Corona Tanzania

January 27, 2021 8:46 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Asema hatarajii kutangaza Watanzania kujifungia ndani ili kujilinda na Corona.
  • Awataka waendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
  • Pia awatahadharisha matumizi ya chanjo ya ugonjwa huo. 

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema hatatangazwa Watanzania wajifungie ndani kwa sababu ya ugonjwa Corona huku akiwataka kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo na kuendelea kumuomba mungu. 

Kauli ya Rais imekujwa wakati kukiwa na mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii ya kuwepo kwa maambukizi ya ugonjwa huo nchini huku baadhi ya taasisi zikiwemo za dini zikiwataka watu wake kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo.

Dk Magufuli aliyekua akizungumza leo Januari 27, 2020 wakati akizindua shamba la miti wilayani Chato mkoani Geita, amesema wakati nchi mbalimbali zikikataza watu wake kutoka nje kujikinga na Corona, Tanzania haitafanya hivyo na watu wake wataendelea kuchapa kazi.

“Nchi nyingi wananchi wake watakua wamejifungia ndani, sisi Watanzania hatujajifungia ndani na hatutegemei kujifungia ndani na wala sitegemei kutangaza hata siku moja kwamba tunajifungia ndani kwa sababu Mungu wetu yuko hai na ataendelea kutulinda Watanzania,” amesema Rais Magufuli 

Licha ya kutojifungia ndani, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari zote zinazopendekezwa na wataalam wa afya dhidi ya ugonjwa huo. 

Pia amewataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kuongeza kasi ya kuzalisha chakula na kufanya mazoezi yatakayowapatia nguvu za kujikinga na virusi vya COVID-19.

“Lakini pia tutaendelea kuchukua tahadhari zingine za kiafya ikiwa ni pamoja na kujifukizia huku unamuomba Mungu huku unapiga zoezi la kufanya kazi, kulima mahindi, viazi ili ule vizuri Corona ishindwe kuingia kwenye mwili wako,” amesisitiza Rais akiwa Chato. 

Amesema Watanzania wameweza kukaa bila Corona kwa zaidi ya mwaka mmoja na hivyo wanatakiwa kuendelea kumuomba Mungu awapiganie na kuwalinda dhidi ya janga hilo. 


Zinazohusiana:


Azungumzia chanjo

Amewataka Watanzania kusimama imara kipindi hiki dhidi ya vitisho vyote vya ugonjwa huo na kuwa makini na chanjo za magonjwa zinazotolewa duniani ikiwemo ya COVID-19. 

“Mtatishwa sana ndugu zangu Watanzania lakini simameni imara. Ninajua wako baadhi ya watanzania wameondoka ndani ya nchi na kukimbilia maeneo mengine na kwenda kuchanjwa na wametuletea Corona ambayo ni ya ajabu. Simameni imara”

“Niombe Wizara ya Afya isiwe inakimbilia mambo ya chanjo bila yenyewe kujiridhisha. Siyo kila chanjo ni amana kwa Taifa letu, siyo kila chanjo ina faida kwetu,” amesema kiongozi huyo wa nchi.  

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV