Hapana: Virusi vya Uviko-19 havipunguzi ukubwa wa uume
- Uviko-19 haushambuli sehemu za siri bali mfumo wa upumuaji.
- Hakuna taarifa rasmi kuthibitisha uzushi huo.
Dar es Salaam. Kama wewe ni miongoni wa watu wanaomini kuwa virusi vya ugonjwa wa Corona (Uviko-19) vinapunguza ukubwa wa uume wa mwanaume, fahamu kuwa hauko katika fikra sahihi.
Ugonjwa huo haushambulii sehemu za siri bali mfumo wa upumuaji wa mtu, hivyo athari zake hujidhihirisha zaidi huko.
Fikra hizo za watu huenda zimetokana na taarifa zisizo sahihi zinazosambaa mtandaoni zikidai kuwa ugonjwa huo ni tishio kwa sehemu za siri za mwanaume.
Taarifa hiyo iliyo katika mfumo wa picha inayosambaa kupitia mtandao wa Twitter ina ujumbe wenye maneno ya Kiingereza “Ujerumani imeripoti virusi vipya vinavyoweza kupunguza uume.”
Baadhi ya wachangiaji wameonyesha kushtushwa na taarifa hizo na kuahidi kuanza kutilia mkazo tahadhari za ugonjwa huo ikiwemo kujitenga.
Ni kweli?
Mpaka sasa hakuna taarifa zozote rasmi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) au wizara ya afya nchini Ujerumani iliyoripoti kuzuka kwa virusi vya Uviko-19 vinavyodaiwa kupunguza saizi ya uume.
Hata hivyo, chanzo cha taarifa hii si cha kuaminika kwa sababu ni habari ya kutengenezwa na watu wenye nia ya kupotosha watu.
Hata hivyo, wananchi wanasisitizwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo kupata chanjo, kunawa mikono mara kwa mara, kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima na kuvaa barakoa.
Latest