Fahamu: Chanjo ya Corona haiongezi ukubwa wa uume

December 11, 2020 4:17 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Madai hayo hayana ukweli wowote kwa sababu wataalam wa afya hawajathibitisha.
  • Chanjo ya Corona bado haijaanza kutumika duniani, iko kwenye majaribio.
  • WHO haijatoa maelezo yoyote kuhusu madhara ya chanjo ya Corona. 

Dar es Salaam.  Wakati watafiti wakiendelea na jitihada za kutafuta suluhu na chanjo ya virusi vya Corona, wapo ambao wanatumia teknolojia kutengeneza taharuki kwenye jamii kwa kutumia ugonjwa huo. 

Moja ya taharuki hiyo ambayo inasambazwa kwenye mmitandao ya kijamii ikiwemo WhatsApp ni uzushi kuwa matumizi ya chanjo dhidi ya Corona yanasababisha uume kuongezeka ukubwa isivyo kawaida. 

Habari hiyo mpasuko (Breaking news) ambayo iko kwenye mfumo wa picha imetengezwa kwenye tovuti ya www.breakyourownnews.com na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Picha iliyotumika kupotosha kuhusu kuongezeka kwa uume baada ya kutumia chanjo ya Corona. Picha|Nukta Fakti

Tovuti hiyo hutumika kutengeneza habari mpasuko zisizo za kweli, lengo ikiwa ni kufurahisha na kutoa utani usiomiza kwenye jamii. 

Moja ya sera ya tovuti hiyo maarufu duniani inaeleza kuwa, “Programu hii ina malengo ya kufurahisha, kuwa makini kwa kile unachotengeneza na jinsi unavyosambaza. Epuka kutengeneza vitu vilivyo kinyume na sheria na vinavyosababisha usumbufu na kuvunja heshima.”

Kutokana na maelezo ya tovuti hiyo, hiyo habari ni ya uongo na aliyetengeneza alilenga kupotosha kama siyo kufurahisha wasomaji. 


Zinazohusiana:


Kuna ukweli wowote kuhusu madai hayo?

Licha ya kuwa habari hiyo imekuja kama mpasuko, haina ukweli wowote na inalenga kupotosha watu ambao wanajiandaa kutumia chanjo kujikinga na janga la COVID-19.

Timu ya Nukta Fakti kwa kutumia zana za kidijitali ikiwemo Google Image Search imebaini kuwa picha hiyo haijatumika sehemu yoyote mtandaoni na hakuna chombo cha habari kilichoripoti kuhusu habari hiyo.

Hata hivyo, mpaka sasa wataalam wa afya likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) bado hawajatoa tamko lolote kuhusu madhara anayoweza kupata mtu endapo atatumia chanjo ya Corona ikiwemo kuongezeka kwa uume (penis enlargement). 

Hata chanjo ambayo Uingereza imeitangaza, bado haijaanza kusambazwa wala kutumika, bali iko kwenye hatua za mwisho ya kuifikisha jamii.

Pia tovuti hiyo ya www.breakyourownnews.com imeeleza kwa uwazi kuwa kama mtu anataka kupata taarifa sahihi za Corona na jinsi ya kujikinga anapaswa kutembelea tovuti ya WHO. 

Kwa vigezo hivyo, habari hiyo haina ukweli, watu wanapaswa kuendelea na maisha yao, wakati wakisubiri taarifa sahihi za wataalam wa afya kuhusu chanjo ya COVID-19.

Enable Notifications OK No thanks