Dk Mwinyi ateua mawaziri, wawili watoka ACT-Walendo

March 3, 2021 2:20 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo Omar Said Shaaban na Nassor Ahmed Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar. 
  • Mwingine ni Dk Saada Mkuya Salum ambaye aliyewahi kuwa  Waziri wa Fedha wa Tanzania 
  • Uteuzi huo unakamilisha Baraza la Mawaziri katika Serikali ya Zanzibar lenye mawaziri 15.

Dar es Salaam. Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Ali Mwinyi  amewateua mawaziri watatu wakiwemo wawili kutoka chama cha ACT-Wazalendo kusimamia wizara tatu visiwani humo. 

Dk Saada Mkuya Salum ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. 

Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, ameteuliwa kuiongoza Omar Said Shaaban ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo. 

Nassor Ahmed Mazrui ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo Zanzibar ameteuliwa kuwa Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

“Uteuzi huo unaanzia leo tarehe 3 Machi 2021,” imeeleza taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena Said,


Soma zaidi:


Rais Mwinyi amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa vifungu vya 42, 43(1)(2) na 44 vya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ambapo wateuliwa hao watatu wanatarajiwa kuapishwa kesho Machi 4.

“Mheshimiwa Rais atamwapisha pia ndugu Salum Yussuf Ali wa Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ambaye alieuliwa Februari 10 mwaka huu,” amesem Said katika taarifa hiyo iliyotolewa leo Machi 3, 2021. 

Uteuzi huo unakamilisha Baraza la Mawaziri katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lenye mawaziri 15. 

Kuingia kwa Shaaban na Mazrui katika baraza hilo la Mawaziri kunafuatiwa kuteuliwa na Dk mwinyi kuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Desemba 7, 2020 ambapo aliacha nafasi mbili katika baraza la mawaziri ambazo zilitakiwa kujazwa na wawakilishi kutoka ACT-Wazalendo.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

🔴LIVE: RAIS SAMIA ANAZINDUA MELI YA KWANZA YA UVUVI WA BAHARI KUU

Nukta TV

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Kwa nini wanawake wako katika hatari zaidi kupata magonjwa ya akili?

Nukta TV

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

🔴LIVE: HOMERA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA BUNGENI

Nukta TV

BENEFIT FROM
Nukta ADS
Advertise with us to reach a wider audience with high conversion rates.
Other Nukta Africa Products
Nukta Habari
Stories that matter
Topics
Inuldge yourself with the topics in Nukta
All
Business
Africa
Contact
Tel
+255 750 881 888
Mail
newsroom@nukta.co.tz
Address
Mwananyamala kwa Kopa Dabe House Dar es Salaam TZ, 14108
Social Media

© 2024 Nukta Africa. All Rights Reserved.