Rais Mwinyi atangaza Baraza la Mawaziri Zanzibar

November 13, 2025 3:22 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Idadi ya wizara imeongezeka kutoka 18 hadi 20 baada ya kuanzishwa kwa wizara mbili mpya. 
  • Nafasi nne za Chama Chama cha ACT wazalendo zaachwa wazi.

Dar es Salaam. Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi, ametangaza rasmi baraza jipya la mawaziri, hatua inayoashiria kukamilika kwa safu kuu ya uongozi wa Serikali ya awamu ya nane muhula wa pili.

Akizungumza katika hafla ya kutangaza Baraza hilo leo Novemba 13, 2025, Dk Mwinyi amesema kuwa uteuzi wa baraza hilo umezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo uwiano wa kijinsia, elimu, uzoefu na uwakilishi wa pande zote za Unguja na Pemba. 

“Vigezo vikuu ni mpangilio wa kila mkoa, sababu nchi yetu ina mikoa mitano, elimu, uzoefu, jinsia kwa idadi inayoendana, visiwa vyetu. Kuna vigezo vingi lakini itoshe kusema kazi hii ugumu uko hapo kuhakikisha kila kigezo kinazingatiwa,” ameeleza Rais Mwinyi.

Katika baraza hilo jipya, idadi ya wizara imeongezeka kutoka 18 hadi 20 baada ya kuanzishwa kwa wizara mbili mpya. 

Kwa mujibu Rais Mwinyi, wizara hizo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (na Ubunifu), iliyotokana na mgawanyo wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, na Wizara ya Vijana, Ajira na Uwezeshaji, iliyoundwa kutokana na mgawanyo wa Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji.

“Lengo langu ni kuhakikisha tunashughulikia changamoto ya ajira kwa vijana na kuwawezesha wananchi katika makundi yote kiuchumi,” amesema Rais Mwinyi.

Aidha, Dk Mwinyi ameeleza kuwa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Kazi na Uwekezaji sasa zitakuwa huru chini ya usimamizi wa mawaziri wao, badala ya kuwa chini ya Ofisi ya Rais kama ilivyokuwa awali.

Mawaziri hawa hapa

Miongoni mwa walioteuliwa ni Dk Sada Mkuya Salum kwenda Ofisi ya Rais Ikulu, Dk Harun Ali Suleiman (Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora), Idrisa Mustafa Kitwana (Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum (Tamisemi), Dk Juma Malik Akil (Wizara ya Fedha na Mipango), na  Sharif Ali Sharif (Wizara ya Kazi na Uwekezaji).

Wengine walioteuliwa ni pamoja na Rahma Kassim Ali (Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi), Lela Mohamed Musa (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali), Riziki Pembe Juma (Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo), na Mudrik Ramadhan Soraga (Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari (na Ubunifu).

Vilevile, Suleiman Masoud Makame (Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Mali Asili na Mifugo), Nadir Abdul Latif Alwardi (Wizara ya Maji, Nishati na Madini), Masoud Ali Mohamed (Wizara ya Uchumi wa Buluu), Dk Khalid Salum Mohamed (Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi).

 Anna Atanas Paul (Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto), na Shabani Ali Othman (Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto).

Aidha, Dk Mwinyi amesisitiza kuwa uteuzi huo umezingatia uwezo, uadilifu na uzalendo wa kila mteuliwa.

 “Tunataka mawaziri wenye kasi, uwajibikaji na uadilifu. Hatutakuwa na uvumilivu kwa wale watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao. Spidi ya awamu ya pili lazima iwe tofauti,” amesema kwa msisitizo.

Rais Mwinyi pia ameeleza kuanzishwa kwa mfumo maalum wa tathmini ya utendaji wa viongozi, Performance Delivery System (PDB), utakaopima ufanisi wa kila wizara.

“Tunataka watu watakao wajibika. Kwa kweli watu waliopata nafasi basi wajue wamepewa jukumu na kila mtu atekeleze jukumu lake,” amefafanu Dk Mwinyi.

ACT milango wazi kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa 

Rais Dk Mwinyi, ameongeza kuwa nafasi nne za uwaziri zimeachwa wazi kwa chama cha ACT Wazalendo, ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Wizara ya Afya na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, hadi pale watakapokubali rasmi kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)

“Kama mnavyoelewa, sheria yetu ya katiba inataka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iwe Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Kwa hiyo, nafasi hizi za uwaziri zimeachwa wazi. Nina matumaini na nina imani kwamba wenzetu wa ACT-Wazalendo wataamua kuja kushiriki kwenye Serikali,” ameeleza Rais Mwinyi katika hotuba yake.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

PART 2: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta.

Nukta TV

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

PART 1: Yafahamu magari 10 yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV