Uzazi wa mpango kufanyika kidijitali

March 3, 2021 6:11 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni matumizi ya app ambayo ya Clue inamsaidia mtu kupanga uzazi salama ili kupata watoto kwa watoto.
  • Pia inawasaidia wanawake kufahamu kwa undani siku zake za hedhi.

Dar es Salaam. Zipo njia mbalimbali ambazo watu wanatumia kupanga uzazi ili kupata idadi ya watoto wanaowataka na namna watakavyopishana. 

Njia hizo ni zile za asili na kisasa (vidonge, sindano, kitanzi, pete, kondomu, kuhesababu kalenda na kumwaga nje) zimekuwa na msaada mkubwa katika kuboresha afya ya mwanamke na watoto. 

Hata hivyo, teknolojia tayari imeingia katika suala la uzazi wa mpango ambapo humuwezesha mtu kupangilia vizuri uzazi wa watoto kwa kutumia mifumo ya kidijitali.

Programu tumishi ya simu (App) ya Clue ni miongoni mwa programu zinazowasaidia watu duniani kupangilia uzazi wa mpango ambayo imeruhusiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA) kuzindua mfumo wake wa uzazi wa mpango wa kidijitali.

Mfumo huo unakuja kwa njia ya App ya Clue ambayo inapatikana katika simu zinazotumia mfumo endeshi wa IOS (iPhone) na Android kwa simu zikiwemo Samsung, HTC na Oppo.

Kwa mujibu wa tovuti ya TechCrunch, app hiyo iliyoanzishwa nchini Ujerumani inatarajiwa kuzindua mfumo huo mwaka huu japo uongozi wa app hiyo haujataja siku rasmi ya uzinduzi.

Kupitia app ya Clue, mtumiaji anaweza kupokea maonyo siku ambazo hapaswi kujamiiana bila kinga. Picha| MobiHealthNews.

Nini kipya katika app ya Clue?

Ni wazi kuwa Clue siyo app ya kwanza inayotoa utabiri wa siku ambazo mwananke anakuwa na uwezo wa kushika ujauzito kwa kutumia takwimu kwani zipo app mbalimbali ikiwemo  app ya Natural Cycles.

Tofauti na Naural cycles ambayo humlazimu mtumiaji kuweka tarifa za hali ya joto la mwili kila siku, Clue inafanya kazi kidijitali zaidi kwani inamhitaji mtumiaji wake kuweka taarifa za mwanzo za mzunguko wake pekee.


Soma zaidi:


App hiyo inamhitaji mtumiaji kuweka taarifa za siku mzunguko wa hedhi unapoanza mara kwa mara ili kumpatia utabiri sahihi na anapaswa kuzingatia maonyo anayopewa na app hiyo. 

Kwa kawaida, app hiyo itamkumbusha mtumiaji siku salama za kujamiiana na kumweleza siku ambazo anatakiwa kutokujamiiana ama kutumia kinga.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la The Verge la nchini Marekani, Clue inasema app yake ni thabiti kama njia ya uzazi wa mpango kwa asilimia 92 endapo mtumiaji atatumia kwa mazoea ikiwemo kusahau kujaza taarifa kwa baadhi ya siku lakini ni thabiri kwa asilimia 97 endapo mtumiaji wake atajaza taarifa zake kama inavyotakiwa.

Mbali na kutumika kama app ya uzazi wa mpango, Clue pia inatumika na wanawake kuwakumbusha mzunguko wa hedhi ili kuwasaidia kujiandaa kwa kununua mahitaji maalumu katika kipindi hicho.

Enable Notifications OK No thanks