Corona: Gazeti la The Standard halijasitisha uchapishaji

March 29, 2021 11:14 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Gazeti hilo limezushiwa kusitisha uchapishaji kutokana na waandishi wake watatu kukutwa na Corona.
  • Kampuni inayomiliki gazeti hilo yasisitiza bado inatoa huduma ikiwemo uchapishaji. 

Dar es Salaam. Kama ni mfuatiliaji na msomaji mzuri wa gazeti la The Standard  la nchini Kenya , huenda umekutana na habari zisizo za kufurahisha juu ya kufungwa kwa gazeti hilo baada ya wafanyakazi wake watatu kukutwa na ugonjwa wa Corona. 

Taarifa hiyo inayosambaa kupitia mitandao ya kijamii hasa wa Twitter haina ukweli wowote kwa sababu uongozi wa kampuni hiyo tayari umekanusha madai hayo na shughuli za gazeti hilo kutoa habari zinaendelea kama kawaida.

Uchunguzi uliofanywa na Nukta Fakti umebaini kuwaa taarifa hiyo iliandikwa na kuchapishwa kwenye akaunti ya Twitter ya gazeti hilo ambayo ni feki na isiyotambulika rasmi. 

Taarifa hiyo inasema “Standard Newspaper temporarily closes city centre newsroom at I&M building after three reporters tested positive for COVID-19”.

Kwa tafsiri isiyo rasmi ya Kiswahili ni kuwa  “Gazeti la The Standard limefunga ofisi zake za uchapishaji zinazopatikana jengo la I&M kwa muda baada ya waandishi wake watatu kukutwa na Corona”.

Baada ya taarifa hiyo kusambaa mitandaoni, kampuni hiyo imetoa taarifa kukanusha madai hayo na imesisitiza kuwa hayana ukweli wowote na bado uchapishaji unaendelea kama kawaida. 

“Uzushi! Tafadhali puuza taarifa zinazosambaa kuwa gazeti la Standard Kenya limefunga kwa sababu ya Corona,” inaeleza taarifa ya kampuni hiyo iliyotolewa Jumamosi ya Machi 27, 2021. 

Gazeti hilo maarufu Afrika Mashariki linamilikiwa na kampuni ya Standard Group ya nchini Kenya.

Kwa sasa, kampuni hiyo ina bidhaa zaidi ya 12 zikiwemo televisheni ya mtandaoni, KTN News na redio Maisha.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW