BOT mbioni kupokea sarafu zisizotumika ili kulinda ubora wake

December 29, 2023 3:27 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kubaainika uwepo wa sarafu nyingi zisizotumika.
  • Zitabadilishwa na noti au kuhifadhiwa kama amana.
  • Zoezi kudumu kwa mwezi mmoja pekee.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imetangaza kuwa iko mbioni kuanza kutoa huduma ya kupokea sarafu (coin) zilizotunzwa kwa muda mrefu bila kutumika kwa wananchi wote au taasisi ili kubadilishwa na noti.

Gavana wa BOT Emmanuel Tutuba katika taarifa yake aliyoitoa leo Disemba 29, 2023 amebainisha kuwa huduma hiyo itatolewa katika ofisi zote za BOT pamoja na benki za biashara nchini kuanzia Januari 2, 2024.

“Hatua hii imechukuliwa kutokana na utafiti uliobaini kuwepo kwa sarafu nyingi za shilingi 200, 100, na 50 ambazo hazitumiki kwa muda mrefu katika mzunguko wa kiuchumi na badala yake zimetunzwa au kuwekwa nyumbani, ofisini, kwenye magari, biashara na taasisi mbalimbali nchini,” amesema Tutuba.

Tutuba ameongeza kuwa huduma hiyo itatolewa kama zoezi maalumu la mwezi mmoja ili kuendelea kulinda ubora wa sarafu dhidi ya uharibifu unaotokea katika mazingira yasiyokuwa salama na kurejesha fedha hizo kwenye mzunguko wa kiuchumi.

 “Hivyo, wananchi wote wenye sarafu za Sh200, 100 na 50 ambazo zimetunzwa bila kutumika kwa muda mrefu na wangependa kuzibadilisha ili kupata noti au kuzitunza kama amana katika akaunti zao, wanaombwa kuziwasilisha kwenye ofisi za BOT au benki za biashara kwa ajili ya kupata huduma hiyo,” amesisitiza Tutuba.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV