Ahueni: Bei ya petroli yashuka kwa Sh102, dizeli Sh101

September 2, 2026 10:06 am · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Sh10,000 sasa itanunua lita 2.63 za petroli Dar es Salaam, kutoka lita 2.57 mwezi uliopita.
  • Nafuu hiyo yatoa ahueni kwa madereva na wafanyabiashara wanaotegemea mafuta katika shughuli zao za kila siku.

Dar es Salaam. Watumiaji wa vyombo vya moto nchini Tanzania huenda wakaanza mwezi Septemba kwa kicheko baada bei ya dizeli na petroli kushuka kwa mwezi wa tatu mfululizo.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) leo Septemba 2, 2026 imesema bei ya rejareja ya petroli imeshuka kwa Sh102 na Sh101 dizeli.

Kwa viwango vipya, lita moja ya petroli inayopitia Bandari ya Dar es Salaam itauzwa kwa Sh3,796 kutoka Sh3,898 mwezi Agosti huku dizeli ikishuka hadi Sh3,877 kutoka Sh3,978.

Mafuta ya taa nayo yanauzwa kwa Sh3,713 kutoka Sh4,003 mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ewura, mabadiliko hayo yametokana na hatua mbalimbali ambazo Serikali imezichukua ili kuwa na bei himilivu za mafuta nchini.

Nafuu ya bei ya mafuta yaendelea

Ahueni hiyo ya mafuta Septemba inaendeleza mwenendo wa kushuka kwa gharama za mafuta nchini kwa miezi mitatu mfululizo, jambo linaloweza kutoa unafuu kwa madereva, wafanyabiashara na sekta nyingine zinazotegemea mafuta katika shughuli za kila siku.

Watumiaji wa vyombo vya moto walianza kuionja shubiri ya kupaa kwa bei ya mafuta mwezi Machi, 2026 baada ya vita vya Marekani, Israel na Iran.

Tangu wakati huo bei ya mafuta duniani ilipaa suala lililosababisha maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto na wananchi wa kawaida baada ya bei ya baadhi ya bidhaa muhimu pia kuongezeka.

Kwa bei mpya za Dar es Salaam, Sh10,000 sasa itanunua lita 2.63 za petroli, ikilinganishwa na lita 2.57 zilizopatikana mwezi Agosti.

Kwa dizeli, kiasi hicho kitamwezesha mtumiaji kupata lita 2.57, kutoka lita 2.51 zilizopatikana kwa Sh10,000 mwezi uliopita.

Je, bei za bidhaa nazo zitashuka?

Pamoja na kushuka kwa bei ya mafuta, unafuu huo huenda usionekane mara moja katika bei za bidhaa na huduma, kwa kuwa wafanyabiashara na wazalishaji huhitaji muda kuendana na gharama mpya za uzalishaji na usafirishaji.

Mtaalamu wa fedha na uchumi kutoka jijini Dar es Salaam Paul Chengula amesema kushuka kwa gharama za mafuta kunaweza kuchangia kushuka kwa gharama za maisha, hasa iwapo gharama za usafirishaji nazo zitapungua.

“‘Kama watu wa transportation (usafirishaji) nao watashusha gharama, ‘automatically’ na gharama za maisha zitashuka kwa kiasi fulani. Lakini mara nyingi watu ‘ku-adjust’ wote kushusha bei kwa mara moja siku moja kama leo inakuwa haiwezekani. Itashuka polepole,” amesema katika mahojiano na Nukta Habari.

Ameeleza kuwa baadhi ya bidhaa huwa zimetengenezwa au kununuliwa wakati bei za mafuta zilikuwa juu, hivyo wafanyabiashara hawawezi kushusha bei mara moja kwa sababu bado wanauza bidhaa zilizotengenezwa kwa gharama za zamani.

“Mfanyabiashara ataziuza kwa gharama ile ile kubwa, lakini huko mbeleni baada ya muda kidogo ndiyo zinaweza zikaja ‘zika-adjust’ kwa pamoja,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Fahamu kuhusu 'BIPOLAR' | Ugonjwa hatari unaoathiri na kubadili hisia

Nukta TV

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Je, ’BIPOLAR’ ina uhusiano na kupenda kufanya tendo la ndoa zaidi?

Nukta TV

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Hii ndio sababu uhusiano wa kimapenzi ni marufuku makazini

Nukta TV