Shilingi ya Tanzania yaendelea kuimarika dhidi ya sarafu za kigeni
- Euro ya Pauni ya Uingereza zashuka kidogo dhidi ya Shilingi Tanzania CRDB na NMB.
Dar es Salaam. Shilingi ya Tanzania imeendelea kuimarika dhidi ya Sarafu inzyotumika katika nchi za umoja wa Ulaya na Pauni ya Uingereza (GBP), kufuatia kushuka kwa viwango vya ununuzi wa sarafu hizo katika Benki za CRDB na NMB, Novemba 16, 2026, ikilinganishwa na Novemba 12, 2026.
Kwa mujibu wa viwango vinavyotumika leo katika Benki ya CRDB, Euro imeshuka kutoka Sh2,793.67 hadi Sh2,774.38, sawa na upungufu wa Sh19.29. Kwa upande wa NMB, kiwango hicho kimeshuka kutoka Sh2,773 hadi Sh2,757, sawa na Sh16.
Vilevile, Pauni ya Uingereza imeshuka katika benki zote mbili. CRDB imeshusha kiwango cha ununuzi kutoka Sh3,369.47 hadi Sh3,350.98, punguzo la Sh18.49, huku NMB kikishuka kutoka Sh3,312 hadi Sh3,295, sawa na Sh17.
Mwenendo huo unaonesha kuimarika kwa Shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu hizo mbili, hali inayoweza kuwa na manufaa kwa wafanyabiashara na waagizaji wa bidhaa kutoka nchi zinazotumia Euro na Pauni, kwa kuwa inaweza kupunguza gharama za kubadilisha fedha wanapofanya malipo ya kimataifa.
Hata hivyo, athari halisi kwa biashara hutegemea pia bei za bidhaa na gharama nyingine za uagizaji.
