Ahueni: Bei ya mafuta yazidi kushuka
- Yashuka kwa mwezi wa pili.
- Serikali yatoa ruzuku kupunguza makali.
Dar es Salaam. Bei ya mafuta imeshuka kwa mara pili mfululizo tangu mwezi Septemba mwaka huu hali inayoendelea kuleta nafuu kwa wamiliki wa vyombo vya moto nchini.
Bei za dizeli, petroli na mafuta ya taa zimeshuka kwa mara ya pili tangu mwezi Septemba mara baada ya kupanda kwa miezi nane mfululizo tangu Januari mwaka 2022.
Nafuu hiyo ya bei ya mafuta kwa mwezi Oktoba imechangiwa na ruzuku ya Sh59.58 bilioni iliyotolewa na Serikali kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta nchini.
Kwa mujibu wa bei kikomo za mafuta za rejareja zinazoanza kutumika leo Agosti 5, 2022 zilizotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakazi wa Jiji la Dar es Salaam wananunua petroli kwa Sh2,886 kwa lita moja ukilinganisha na Sh2,969 iliyokuwa ikitumika mwezi Septemba mwaka huu.
Ahueni hiyo ya mafuta kwa mwezi Oktoba kwenye mafuta ya petroli ni ya Sh83 ambayo ni kwa mafuta yanaoingia nchini kupitia bandari ya Dar es Salaam.
Wakati bei ya petroli ikishuka, bei ya mafuta ya dizeli nayo imeendelea kuporomoka ambapo inauzwa kwa Sh3,083, kutoka Sh3,125 ya mwezi uliopita huku mafuta ya taa yakiuzwa kwa Sh3,275 kwa lita kutoka Sh3,335 kwa lita mwezi Septemba.
Kulingana na taarifa hiyo kushuka kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hizo katika soko la dunia kwa Agosti 2022, ambazo zimetumika katika kukokotoa bei za mafuta za hapa nchini katika mwezi wa Oktoba 2022.
Zimepungua kwa asilimia 7.4, 3.9 na 1.9 kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, mtawalia, ikilinganishwa na bei hizo kwa mwezi Julai 2022.
Zinazohusiana
Licha ya bei hizo kushuka, wakazi wa Ruberwa, Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera ndiyo wananunua petroli kwa bei ya juu kuliko maeneo mengine nchini.
Bei ya petroli katika eneo hilo ni Sh3,124 kwa lita moja.
Bei ya dizeli kupitia bandari ya Mtwara imeshuka kufikia Sh2,908 na Sh3,099 (petroli) huku mafuta yanayoingia kupitia bandari ya Tanga yakifikia Sh2,924(dizeli) na Sh3,108 (petroli).
Sababu za kushuka kwa bei za mafuta zatajwa
Kulingana na taarifa hiyo kushuka kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hizo katika soko la dunia kwa Agosti 2022, ambazo zimetumika katika kukokotoa bei za mafuta za hapa nchini
Mwezi wa Oktoba 2022 zimepungua kwa asilimia 7.4, 3.9 na 1.9 kwa mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, mtawalia, ikilinganishwa na bei hizo kwa mwezi Julai 2022.
Hata hivyo, ikilinganishwa na gharama za uagizaji zilizotumika katika kukokotoa bei za Septemba 2022, gharama za uagizaji wa mafuta zimeongezeka kwa kati ya asilimia 50 na 163 kwa kutegemea bandari na bidhaa husika ikilinganishwa na gharama za uagizaji zilizotumika katika kukokotoa bei za Septemba 2022, na hivyo kuathiri mwenendo wa bei za mafuta hapa nchini.
“Pamoja na hayo, kufuatia dhamira ya Serikali ya kuendelea kupunguza madhara ya ongezeko la bei za mafuta hapa nchini kwa wananchi na uchumi kwa ujumla, Serikali imetoa ruzuku ya Sh59.58 bilioni kwa ajili ya bei za mafuta ya Oktoba 2022,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Ewura Modestus Lumato.
Latest