Bei za petroli, dizeli zaendelea kushuka Tanzania

February 7, 2024 7:45 am · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Petroli yashuka kwa Sh33 kwa lita kwa bei ya rejareja, dizeli kwa Sh49 na mafuta ya taa kwa Sh670 kwa lita.
  •  Ahueni hiyo inatokakana na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa wastani (weighted average).

Dar es Salaam. Maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto nchini yameendelea kupungua kidogo kwa mwezi Februari mara baada ya bei ya mafuta ya Petroli na dizeli kushuka kwa mwezi wa tano mfululizo.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Tanzania (Ewura) leo Februari 7, 2024 inaeleza kuwa bei ya rejareja ya petroli iliyoingizwa kupitia Bandari ya Dar es Salaam imeshuka kwa Sh33 kwa lita huku ile ya dizeli ikipungua kwa Sh49 kwa lita.

Ahueni hiyo imeenda hadi kwenye katika mafuta ya taa ambayo bei yake imeshuka kwa Sh670 kwa lita.

Katika bei hizo mpya, wakazi wa Dar es Salaam watanunua petroli kwa reja reja kwa Sh3,051 kwa lita kutoka Sh3,084 iliyotumika mwezi Januari huku dizeli ikinunuliwa kwa Sh3,029 kwa lita kutoka 3,078 iliyorekodiwa mwezi uliopita. Mafuta ya taa sasa Dar es Salaam yatauzwa Sh2,840 kwa lita kwa bei ya rejareja kutoka Sh3,510 iliyotumika Januari 2024.

Kwa upande wa mafuta yanayoingizwa kupitia Bandari ya Tanga  lita moja ya petroli itanunuliwa kwa Sh3,064 ambayo ni bei sawa na iliyorekodiwa  mwezi Januari, dizeli kwa Sh3,196 kutoka Sh3,219  na mafuta ya taa kwa Sh2,886 kutoka Sh3,556 iliyorekodiwa mwezi uliopita.

Bandari ya Mtwara watanunua mafuta hayo kwa petroli Sh3,112 kwa lita, kutoka Sh3,201 mwezi Januari mwaka huu, dizeli Sh3,354 kutoka Sh3,456  na mafuta ya taa Sh2,913 kutoka 3,582 mwezi uliopita.


Soma zaidi:Deni la Tanroads kitendawili kingine Serikali ya Rais Samia


Wakazi wa Kyerwa (Ruberwa) mkoani Kagera ndio wanaonunua mafuta hayo kwa bei ya juu zaidi ya Sh3,288 kwa petroli, kwa upande wa dizeli wakazi wa Nyasa (Mbamba Bay) mkoani Ruvuma ndio wanaonunua nishati hiyo kwa bei ya juu zaidi ya Sh3,477.

Wakazi wa Dar es Salaam ndiyo wenye ahueni zaidi baada ya petroli kuuzwa kwa Sh3,051 na dizeli kwa Sh30,29 ikiwa ni kiwango chacha chini zaidi ya mikoa mingine.

Kwa mujibu wa Ewura, kupungua kwa bei za mafuta kwa mwezi Februari 2024 kunatokana na kushuka kwa bei za mafuta (FOB) katika soko la dunia kwa wastani (weighted average) kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa.

“Pia kupungua kwa bei za mafuta kumetokana na kushuka kwa gharama za uagizaji wa mafuta kwa Bandari ya Dar es Salaam kwa wastani (weighted average) wa asilimia 9.69 kwa dizeli na asilimia 1.82 kwa mafuta ya taa,” imesema taarifa ya Ewura. 

Hata hivyo, ahueni hiyo katika bei ya mafuta nchini haitoshi kupooza maumivu kwa watumaiji wa nishati hiyo inayohitajika zaidi katika kuendeleza shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.


Soma zaidi:Watoto wadogo katikati ya kuisaka elimu madarasa ya awali Tanzania-2


Mathalan, mtumiaji aliyekuwa anatumia Sh10, 000 kupata lita 3.24 za petroli kwa bei mpya iliyotangazwa leo atapata lita 3.27 za mafuta ongezeko ambalo halitaweza kusogeza chombo chake cha usafirihata kwa hatua moja. 

Kwa watumiaji wa dizeli hali ni hiyo hiyo, kwa bei mpya ya leo akiwa na  Sh10,000 atapata lita 3.3 kutoka lita 3.2 alizokuwa anapata mwezi Januari.

Kushuka kwa bei ya mafuta kwa miezi miezi mitano mfululizo tangu Oktoba, 2023 iwapo mwenendo huo ukaendelea kwa miezi mingine ijayo utaendelea kuwapatia ahueni wa watumiaji wa vyombo vya moto ambao hulazimika kutoboa mifuko yao zaidi kuipata nishati hiyo.

Mwezi Julai, 2023 ndio ulioshuhudia bei ndogo zaidi ya nishati hiyo kabla ya kupanda kwa takribani miezi mitatu kati ya mwezi Agosti, Septemba na Novemba.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV