Michezo, burudani vyachangia kupaisha mfumuko wa bei Tanzania

February 8, 2021 3:45 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 3.5 mwaka ulioshia Januari 2021 kutoka 3.2 Desemba, 2020.
  • Bidhaa za chakula zashuka bei huku huduma za burudani, michezo na utamaduni zikipanda.
  • Huduma zingine zilizopanda bei ni pamoja na huduma za makazi, maji, umeme na gesi.

Dar es Salaam. Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Januari 2021 umeongezeka kidogo hadi kufikia asilimia 3.5 kutoka asilimia 3.2 iliyorekodiwa mwaka ulioishia Desemba mwaka jana ukichagizwa zaidi na kupaa kwa bei za baadhi ya bidhaa na huduma za usafiri na afya. 

Taarifa ya mfumuko wa bei iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Februari 8, 2021 inaeleza bei za huduma za burudani, michezo na utamaduni zimeongezeka kwa asilimia 3.2 huku gharama za samani za nyumbani na ukarabati zikiongezeka kwa asilimia 2.2 zikiwa sawa sawa na bidhaa za usafi binafsi na wa kijamii.


Soma zaidi:


Bidhaa nyingine na huduma zilizopanda katika kipindi hicho ni huduma za makazi, maji, umeme, gesi na mafuta mengine kwa asilimia 1.1 na huduma za usafiri kwa asilimia 1.5. 

NBS imeeleza kuwa bidhaa nyingine zilizopanda bei ni mavazi na viatu ambavyo vimepanda kwa asilimia 1.9 huku pombe na bidhaa za tumbaku zikipanda kwa asilimia 0.6

Hata hivyo, kasi ya mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi ulishuka kidogo katika katika kipindi hicho. 

“Mfumuko wa bei za vyakula na vinywaji baridi umeshuka kutoka asilimia 3 mwezi Desemba, 2020 hadi asilimia 2.8 mwezi Januari 2021,”  inasomeka sehemu ya taarifa iliyotolewa na NBS.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV