NAS, shirika la ndege la Ufaransa wasaini mkataba kutoa huduma za usafiri wa ndege Tanzania

Ndege ya shirika la ndege la Ufaransa la KLM ambalo limeingia makubaliano na NAS kuanza kutoa huduma za usafiri Tanzania. Picha| Mtandao.
- Hatua hiyo ni kuongeza ushindani na kuimarisha sekta ya usafiri wa ndege nchini.Â
- Shirika hilo litakuwa na kibarua kigumu cha kushindana na mashirika mengine ya Air Tanzania, Precision Air, Rwand Air, Fly Dubai na Ethiopian Airlines ambayo yamejiimarisha hapa nchini.Â
- NAS inakusudia kuongeza uwekezaji wake hadi Sh23 bilioni katika sekta ya usafiri wa anga nchini.
Dar es Salaam. Kampuni ya  huduma za usafiri wa anga (NAS) imeingia mkataba na shirika la ndege la  Ufaransa (Air France-KLM)  kuanza kutoa huduma za usafiri wa ndege Tanzania ili kuongeza ushindani na kusaidia kukuza soko la usafiri wa anga nchini.Â
Kwa mujibu taarifa ya NAS iliyotolewa leo (Aprili 2, 2019) imeeleza kuwa kutokana na uzoefu wa kampuni hizo mbili katika utoaji wa huduma za usafiri wa ndege kimataifa, utasaidia kuimarisha huduma za usafiri wa anga nchini.Â
Shirika la ndege la ufaransa KLM linakua shirika la sita kuingia nchini kwa ajili ya kutoa huduma za usafiri wa anga ambapo litakuwa na kibarua kigumu cha kushindana na mashirika mengi ya Air Tanzania, Precision Air, Rwanda Air, Fly Dubai na Ethiopian Airlines ambayo yamejiimarisha hapa nchini.Â
 Air France-KLM imekuja katika kipindi ambacho kampuni ya ndege ya Fastjet ikiwa imeondoka sokoni kutokana na kukabiliwa na changamoto za uongozi na uendeshaji. Fastjet ilikuwa ikisifika kwa huduma bora ikiwemo nauli zenye gharama nafuu kwa wateja wake, jambo lililovutia watanzania wengi kutumia usafiri huo.Â
Lakini kwa sasa, ushindani unaonekana zaidi kwa Air Tanzania na Precision Air ambazo zimetawala soko la ndani hasa katika mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya, Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma.Â
Soma zaidi:
- Airbus yatundika daruga kutengeneza ndege za kifahari za Airbus A380 Superjumbo
- Mambo unayotakiwa kufanya ukifika mapema ‘Airport’
- Shirika la ndege la Ethiopia limesitisha safari zote za ndege aina ya Boeing 737
Mwaka 2018 NAS DAR (AIRCO)  ambayo inatoa huduma za usafiri katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) walipokea ndege 7,000, mizigo 467,000, tani 700 za mizigo mikubwa  na kuhudumia wateja 515,000 katika viwanja vya ndege vya Dar es Salaam, Kilimanjaro na Dodoma kufikisha asilimia 98.9 ya utendaji kazi wa ndege (OTP).
Hiyo ina maana kuwa kuna ongezeko la asilimia 43 la shughuli za uendeshaji wa kampuni hiyo ukilinganisha na mwaka 2017.
Mwaka huu wa 2019, NAS ina mpango wa kuongeza uwekezaji wake wa Dola za Marekani 10,000,000 (Sh23 bilioni) nchini Tanzania ili kuendeleza sekta ya anga.
Latest