Wanaotumia usafiri wa ndege waongezeka Tanzania

October 7, 2022 12:36 pm · Abdushakur
Share
Tweet
Copy Link
  • Mwaka 2021 walikuwa milioni 3.8 wakiongezeka kutoka milioni 2.7 wa mwaka 2020. 
  • Kuimarika kwa sekta ya anga baada ya Uviko-19 kwachangia.

Mwanza.  Idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini Tanzania imeongezeka kwa asilimia 38 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja, baada ya kuimarishwa kwa mapambano dhidi ya Uviko-19.

Kwa mujibu wa Kitabu cha Hali ya Uchumi kwa mwaka 2021 kilichotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), idadi ya abiria waliotumia usafiri wa anga nchini mwaka 2021 walikuwa milioni 3.8 wakiongezeka kutoka milioni 2.7 wa mwaka 2020.

Hilo ni sawa na ongezeko la abiria milioni 1.1 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. 

Kati ya abiria hao, milioni 2.3 sawa na asilimia 60.5 walikuwa abiria wa ndani. 

Tangu mwaka 2017 hadi 2021 idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa anga nchini imekuwa ikipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kusitishwa kwa muda kwa safari za ndege mwaka 2020 kutokana na janga la Uviko-19. 

Mathalan, Mwaka 2017 abiria waliotumia usafiri huo walikuwa milioni 5 na mwaka uliofuata waliongezeka hadi milioni 5.1 kabla hawajaongezeka zaidi hadi milioni 5.4.

Hata hivyo, mwaka 2020, idadi hiyo ilishuka mara mbili hadi milioni 2.7.


Soma zaidi: 


“Kutokana na katazo la safari za anga kufuatia mlipuko wa Uviko-19, jumla ya mashirika 21 ya kimataifa ya ndege yalifuta safari 632 zilizopangwa kufanyika kuja nchini kuanzia tarehe 20 Machi 2020,” imeeleza sehemu ya kitabu hicho.

Hatua hiyo ilisababisha kudorora kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi hususan biashara na huduma kama usafirishaji wa chakula, vinywaji na burudani.

Baada ya hatua mbalimbali kuchukuliwa kukabiliana na Uviko-19 ikiwemo utoaji wa chanjo na kulegezwa kwa masharti ya safari za kimataifa, kumesaidia sekta ya anga kuimarika siku za hivi karibuni. 

Tangu alipoingia madarakani Machi 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alieleza kuwa Serikali imedhamiria kuhuisha shughuli za usafiri wa anga nchini ikiwemo Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kujiendesha kibiashara na kulipunguzia mzigo wa madeni.

Mpaka sasa, Serikali ina ndege 11 zinazofanya safari za ndani na nje ya nchi ambapo mwaka huu wa 2022/23 ina mpango wa kufanya ununuzi wa ndege nyingine tano ili kuongeza ufanisi wa shirika hilo.

Ndege zitakazonunuliwa: moja ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, ndege mbili ni aina ya Boeing 737-9, ndege moja ya mizigo aina ya Boeing 767-300F na ndege moja aina ya Dash 8 Q400.

Huenda ujio wa ndege hizi utaongeza ushindani katika sekta ya anga nchini na hivyo kuongeza idadi ya abiria wanaotumia usafiri wa anga ili kuingizia Serikali mapato mengi zaidi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV