Michelle Kilpin wa TBL achaguliwa Bodi ya AmCham Tanzania
- AmCham Tanzania ni chama cha wafanyabiashara na wawekezaji kinacholenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Marekani.
Dar es Salaam.Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Michelle Kilpin, amechaguliwa kuwa mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya American Chamber of Commerce in Tanzania (AmCham Tanzania), hatua inayolenga kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Marekani.
American Chamber of Commerce in Tanzania (AmCham Tanzania) ni chama cha wafanyabiashara na wawekezaji kinacholenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Marekani pamoja na kukuza mazingira bora ya uwekezaji nchini.Â
Kupitia nafasi hiyo mpya, Michelle anatarajiwa kuchangia uzoefu wake katika masuala ya uongozi wa biashara, uwekezaji na uendelezaji wa mazingira rafiki kwa biashara ndani ya AmCham Tanzania, taasisi inayolenga kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Marekani.
Michelle Kilpin aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) mwezi Februari 2024, na kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo katika historia ya miaka 90 ya kampuni hiyo.Â
Kabla ya kujiunga na TBL, alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Zambia Breweries Limited, ambako ameacha alama ya uongozi kwa kukuza mapato na kuongeza uwekezaji wa kampuni hiyo.
Pia ana uzoefu wa zaidi ya miaka 19 ndani ya kampuni mama ya TBL, AB InBev, akifanya kazi katika nafasi mbalimbali za uongozi barani Afrika.Â
TBL imesema uteuzi wake ndani ya AmCham Tanzania unaonyesha imani ya wadau wa biashara kwa uongozi wa Michelle na mchango wake katika kujenga thamani ya muda mrefu kwa kampuni, jamii na uchumi kwa ujumla.