Idadi ya Watanzania yaongezeka kwa asilimia 3.03 kwa mwaka mmoja

June 19, 2019 11:55 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Wakati idadi ya Watanzania ikiongezeka kwa asilimia 3.03, mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na watu wengi zaidi wapatao milioni 5.1 sawa na asilimia 9.8 ya watu wote Tanzania Bara.Picha|Mtandao.


  • Watu waliongezeka ni milioni 1.64 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja na kuifanya Tanzania iwe na watu milioni 54.14.
  • Mkoa wa Dar es Salaam bado unaongoza kwa kuwa na wati wengi.
  • Huduma bora za kijamii ndio kivutio kikubwa cha watu kuja Dar es Salaam.
  • Katavi, Njombe na Lindi bado zina idadi ndogo ya watu Tanzania Bara. 

Dar es Salaam. Katika kipindi cha mwaka mmoja inakadiriwa kuwa  idadi ya Watanzania imeongezeka kwa asilimia 3.03 huku mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kuwa na idadi kubwa ya watu, jambo linatoa changamoto katika uboreshaji wa huduma muhimu za jamii ikiwemo afya na maji. 

Mwaka jana, mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na watu wengi zaidi wapatao milioni 5.14 sawa na asilimia 9.8 ya watu wote Tanzania Bara.  

Kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018, kilichotolewa Juni mwaka huu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kinaeleza kuwa hadi kufikia Desemba 2018, idadi ya watu Tanzania ilikadiriwa kuwa milioni 54.19 ikilinganishwa na watu milioni 52.55 mwaka 2017.

Watu walioongezeka ni milioni 1.64 au sawa na ongezeko la asilimia 3.03 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. 

“Kati ya hao, wanawake walikadiriwa kuwa milioni 27.68 sawa na asilimia 51.1 ya watu wote na wanaume milioni 26.51 sawa na asilimia 48.9. Aidha, Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu milioni 52.61, sawa na asilimia 97.1 ya watu wote na Tanzania Zanzibar watu milioni 1.57,” inasomeka sehemu ya kitabu hicho.

Kwa mujibu wa takwimu za kitabu hicho, makadirio hayo yalitokana na matokeo ya idadi ya watu kwa kutumia matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na viashiria muhimu vya mabadiliko ya idadi ya watu vikijumuisha uzazi, vifo na uhamiaji,” inaeleza sehemu ya kitabu hicho. 


Soma zaidi: Vijue vipaumbele vya Watanzania wanapopata pesa


Wakati idadi ya Watanzania ikiongezeka kwa asilimia 3.03, mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na watu wengi zaidi wapatao milioni 5.1 sawa na asilimia 9.8 ya watu wote Tanzania Bara.

 Idadi kubwa ya watu katika mkoa wa Dar es Salaam ilitokana na upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii na za kiuchumi na hivyo kusababisha ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaohamia kutoka mikoa mingine. 

Hiyo ni ishara kuwa juhudi bado zinahitajika kuboresha zaidi huduma za jamii na kiuchumi katika maeneo mbalimbali nchi ili kuendelea kumudu mahitaji ya ongezeko la watu. 

Aidha, mkoa wa Katavi ulikuwa na idadi ndogo zaidi ya watu ikilinganishwa na mikoa mingine ya Tanzania Bara, ukikadiriwa kuwa na watu 738,237 sawa na asilimia 1.4, ukifuatiwa na mikoa ya Njombe na Lindi iliyokuwa na watu 803,299 na 983,738 mtawalia. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV