Pato la Mtanzania laongezeka kwa Sh244,487 mwaka 2025

June 11, 2026 12:22 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Sasa wastani wa pato la mtu mmoja mmoja Tanzania (GDP per capita) limefikia Sh3.5 milioni mwaka 2025

Dar es Salaam. Wastani wa pato la mtu mmoja mmoja nchini Tanzania (GDP per capita) limeongezeka kwa Sh244,487 ndani ya mwaka mmoja hadi kufikia Sh3.5 milioni mwaka 2025, kiwango cha juu kuwahi kurekodiwa nchini. 

Ongezeko hilo, kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo ni asilimia 7.4 kutoka takriban Sh3.3 milioni iliyorekodiwa mwaka 2024. 

Katika viwango halisi baada ya maboresho ya mwaka kizio wa Pato la Taifa (GDP) kuwa 2019 badala ya 2015, pato la mmoja mmoja lilikuwa 3,544,124 mwaka 2025 kutoka Sh3,299,637 mwaka 2024.

Profesa Mkumbo ameliambia Bunge wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa Taifa ongezeko la pato hilo limechagizwa zaidi na ukuaji wa pato la Taifa ambalo kwa sasa limefikia Sh234.1 trilioni.

Wastani wa pato la mtu mmoja mmoja (GDP per capita) ni kipimo kinachoonesha kiasi cha thamani ya bidhaa na huduma zote zinazozalishwa katika nchi ndani ya kipindi fulani, kilichogawanywa kwa idadi ya watu wa nchi hiyo.

Kwa kifupi, wastani huu unapatikana kwa kuchukua Pato la Taifa ambalo kwa sasa ni Sh234.1 trilioni kwa kugawanya na jumla ya idadi ya Watanzania ambao kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wanakadiriwa kuwa milioni 70.

Mwaka 2025, uchumi wa Tanzania ulikua kwa kasi ya asilimia 5.9 kutoka asilimia 5.6 iliyorekodiwa mwaka 2024. Katika mwaka 2026, Serikali inatarajia uchumi utakua kwa asilimia 6.3 licha ya presha kubwa ya kuongezeka gharama za bidhaa na huduma kutokana na vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran. 

Profesa Mkumbo ameeleza kuwa ukuaji wa pato la Taifa umechangiwa na kukua kwa uchumi wa sekta mbalimbali ikiwemo kilimo iliyoongoza kwa kuchangia asilimia 24.3 ya pato.

“Sekta zilizokuwa na mchango mkubwa katika Pato la Taifa zilikuwa kilimo, ikifuatiwa na ujenzi asilimia 11.9, uchimbaji madini na mawe (asilimia 10.3), biashara na matengenezo asilimia 8.6 na usafirishaji na uhifadhi wa mizigo asilimia 8.3,” amesema Profesa Mkumbo.

‘Si kipimo halisi’

Wastani wa pato kwa Mtanzania umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka. Hata hivyo, licha ya kuongezeka kwa pato hilo Watanzania wengi bado wamekuwa wakilalamikia hali ngumu ya maisha, kipato duni huku wakikabiliwa na mfumuko wa bei ambao umekuwa kwa asilimia 4.2 kwa mwaka ulioishia Mei 2026.

Huenda hali hii inatokana na ukweli kwamba GDP per capita si kipimo cha moja kwa moja cha kipato halisi anachopokea kila Mtanzania, bali ni wastani wa takwimu unaojumuisha kipato cha walionacho na wasionacho.

Mtaalamu wa masuala ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Kinyondo, aliwahi kuieleza Nukta Habari kuwa wananchi hawapaswi kutafsiri GDP per capita kama fedha wanazopaswa kuzipokea moja kwa moja, kwa kuwa kipimo hicho si kipimo cha mapato halisi ya kaya au watu binafsi.

“Wanachukua jumla ya kipato cha mtu mwenye fedha nyingi ambaye anauwezo wa kuingiza mabilioni kwa mwaka alafu wanagawanya kwa kumjumlisha na mkulima mmoja mwenye maisha duni ambaye hana hata uwezo wa kuingiza milioni kwa mwaka,” alisema Profesa Kinyondo.

Kwa maana hiyo, hata kama wastani wa pato la mtu mmoja mmoja unaongezeka, faida za ukuaji wa uchumi zinaweza zisigawanyike kwa usawa miongoni mwa wananchi. Watu wachache wenye kipato kikubwa wanaweza kuongeza wastani huo, ilhali sehemu kubwa ya wananchi ikiendelea kupata kipato cha chini. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
12 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
12 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
12 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV