Bajeti wizara ya habari yaongezeka kwa Sh9.4 bilioni

April 23, 2020 10:43 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Bajeti ya wizara hiyo ya mwaka 2021/2021 imeongezeka hadi Sh40.2 bilioni kutoka Sh30.8 bilioni mwaka huu. 
  • Itatumika kuratibu na kusimamia maendeleo ya sekta za habari, utamaduni, sanaa na michezo na taasisi zake.

Dar es Salaam. Bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  ya mwaka 2021/2021 imeongezeka kwa Sh9.4 bilioni na kufikia Sh40.2 bilioni zitakazotumika kipindi hicho kuratibu na kusimamia maendeleo ya sekta za habari, utamaduni, sanaa na michezo na taasisi zake. 

Bajeti hiyo iliyosomwa Bungeni jana (Aprili 22, 2020) na kupitishwa na wabunge imeongezeka kutoka Sh30.8 ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 sawa na ongezeko la Sh9.4 bilioni ndani ya kipindi cha mwaka mmoja. 

Waziri wa wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe aliyekuwa akisoma hotuba hiyo, amesema kati ya fedha hizo, Sh20.9 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi wa wizara huku Sh11.5 bilioni zitaelekezwa katika matumizi mengineyo. 

Dk Mwakyembe amesema Sh7.7 bilioni sawa na asilimia 3.1 ya bajeti yote itaenda katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo. 


Zinazohusiana: 


Amesema bajeti hiyo ya mwaka 2020/21 itajikita katika kuratibu na kusimamia maendeleo ya sekta za habari, utamaduni, sanaa na michezo na taasisi zake ambapo majukumu mbalimbali yamepangwa kutekelezwa. 

“Tutaimarisha makusanyo ya mapato yatokanayo na shughuli zinazofanyika katika viwanja vya Taifa na Uhuru ambavyo vinamilikiwa na Serikali ikiwemo kuboresha mfumo wa ukusanyaji mapato katika viwanja hivyo,” amesema Dk Mwakyembe. 

Mbali na kuidhinishiwa Sh40.2 bilioni, wizara hiyo itatumia vyanzo vyake kukusanya mapato ya Sh960 milioni kupitia Idara ya Habari-MAELEZO na maendeleo ya michezo. 

“Aidha, kwa upande wa taasisi saba zilizo chini ya wizara kiasi kinachokadiriwa kukusanywa ni jumla ya Sh40.2 bilioni kwa mwaka 2020/21,” amesema Mwakyembe. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV