5G inasambaza corona? Hapana, ni uzushi

May 6, 2020 10:13 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Virusi vya ugonjwa wa corona (COVID-19) haviwezi kusambaa kupitia mawimbi ya redio au mfumo wowote wa mawasiliano ya simu.

Dar es Salaam. Kumekuwa na habari zinasambaa kwa kasi mtandaoni kuwa teknolojia mpya ya mawasiliano ya 5G inasambaza virusi vya corona, hata hivyo, taarifa hizo hazina ukweli wowote kisayansi.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) virusi vya ugonjwa wa corona (COVID-19) haviwezi kusambaa kupitia mawimbi ya redio au mfumo wowote wa mawasiliano ya simu.

Ikumbukwe ugonjwa huo unasambaa kwa kasi hata kwenye mataifa ambayo hayana teknolojia hiyo ya 5G.

“COVID-19 inasambazwa kupitia majimaji ya mtu anapopiga chafya, kukohoa au kuzungumza. Watu wanaweza pia kuambukizwa virusi hivyo kwa kugusa maeneo yenye virusi halafu baadaye wakagusa pua, macho na midomo yao,” WHO inaeleza.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Ujumbe mzito wa Dk. Tulia Ackson kuhusu usawa akiaga urais wa IPU

Ujumbe mzito wa Dk. Tulia Ackson kuhusu usawa akiaga urais wa IPU

Nukta TV

IPU 153 yafungua fursa kwa vijana kupitia matumizi sahihi ya AI na uongozi

IPU 153 yafungua fursa kwa vijana kupitia matumizi sahihi ya AI na uongozi

Nukta TV

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV