Uzushi: Kushiriki ngono mara kwa mara hakuzuii Corona

January 30, 2021 8:29 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Njia sahihi ya kujilinda dhidi ya Corona ni kuvaa barakoa, kunawa mikono na kukaa umbali wa mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine.
  • Ngono inaongeza uwezekano wa kupata Corona kuliko kuzuia.

Dar es Salaam. Kama ni miongoni mwa watu ambao wamekutana na habari mtandaoni inayohamasisha watu kushiriki ngono mara kwa mara ili kujikinga na Corona, fahamu wazi kuwa unadanganywa kwa sababu hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusu dhana hiyo.

Kwa sasa katika mitandao ya kijamii hasa WhatsApp inasambaa picha yenye maneno yanayodai kuwa dawa ya virusi vya Corona imegunduliwa ambapo watu wanatakiwa kufanya mapenzi mara kwa mara ili kujikinga na ugonjwa huo, jambo si la kweli.  

Habari picha hiyo ni uzushi unaolenga kupotosha watu. 

Habari hiyo yenye picha ya Mtangazaji wa Shirika Habari la CNN la Marekani Wold Blitzer inaonyesha sehemu ya habari mpasuko (Breaking News) ikiwa na maelezo kwa lugha ya Kiengereza kuwa “constant sex kills coronavirus” ikimanisha kuwa “kufanya mapenzi mara kwa mara kunaua virusi vya Corona”.  

Mpaka sasa hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha madai hayo.  Mamlaka za afya likiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO) halijatoa tamko lolote kuhusu dhana hiyo, zaidi ya kuwataka watu kuchukua tahadhari zinazopendekezwa na wataalam wa afya ikiwemo kuvaa barakoa. 

Tahadhari nyingine ni kukaa umbali mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine.

Katika kipindi ambacho Corona imeleta taharuki duniani, ni vema kupata taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huo kutoka katika vyanzo sahihi ikiwemo WHO ili kujiweka salama zaidi. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV