Hapana! kuoga maji ya moto siyo kinga dhidi ya Corona

May 22, 2020 9:03 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Maji ya moto hayawezi kukinga na maambukizi ya COVID-19.
  • WHO imesema hata ukioga maji ya moto, joto la mwili hubaki katika hali yake ya kawaida.

Dar es Salaam. Kutokana na janga la virusi vya ugonjwa wa Corona (COVID-19) kuitesa dunia, zimeibuka dhana potofu za kutibu ugonjwa huo ikiwemo kuoga maji ya moto. 

Hata hivyo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema siyo kweli kuoga maji ya moto kunatibu Corona kama inavyodhaniwa na baadhi ya watu. 

Limesema licha ya kuoga maji ya moto, joto la mwii wako litabaki katika hali yake ya kawaida ambayo ni kuanzia sentigredi 36.5 hadi sentigredi 37.

Ikiwa utaoga maji ya moto sana, unaweza kuungua na kuishia kupata gharama za kujitibu majeraha utakayopata.


Zinazohusiana:


Ili kujikinga na COVID-19 unashauriwa kufuata maelekezo ya wataalam wa afya ikiwemo kukaa umbali wa walau mita moja kati yako na jirani yako, kunawa mikono kwa maji tiririka au kutumia vitakasa mikono vilivyothibitishwa. 

Pia epuka kugusa pua, mdomo au macho na mikusanyiko isiyo ya lazima, 

Tahadhari hizo zitakusaidia kujikinga na ugonjwa huo ambao umeenea katika nchi mbalimbali duniani. 

Usiogope! Corona inazuilika na kutibika.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
31 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
31 May, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

AKILI UNDE INAVYOIMARISHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Nukta TV

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

WAFAHAMU 'THE BIG FIVE' WA AFRIKA

Nukta TV

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

HIVI NDIVYO UNAWEZA KUSAFISHA MENO YAKO

Nukta TV