Usidanganyike! Pilipili hazitibu ugonjwa wa Corona

June 20, 2020 9:25 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ingawa pilipili ni zao linalotumika kuongeza ladha kwenye chakula lakini haitibu au kuzuia COVID-19. 
  • Njia rahisi ya kujikinga na Corona ni kukaa mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine, kunawa mikono mara kwa mara na kutumia kitakasa mikono.

Dar es Salaam. Katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa corona habari nyingi za uzushi zimesikika kuhusu namna ya kijitibu na maradhi hayo. 

Moja ya uzushi huo ni baadhi ya watu kudai kuwa matumizi ya pilipili kwenye supu na vyakula vingine yanasaidia kutibu ugonjwa wa COVID-19. 

Kama umekutana au kusoma habari kama hiyo, fahamu kuwa haina ukweli wowote kwa sababu pilipili haitibu ugonjwa huo na hadi sasa kinachofahamika ni kwamba corona haitibiki bali madaktari hutibu tu dalili. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema ingawa pilipili ni zao linalotumika kuongeza ladha kwenye chakula lakini haitibu au kuzuia COVID-19. 

“Kuongeza pilipili kwenye supu au vyakula vingine haizuii au kutibu COVID-19,” imeeleza WHO. 


Zinazohusiana


Njia rahisi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo ni kukaa mita moja kutoka mtu mmoja na mwingine, kunawa mikono mara kwa mara na kutumia kitakasa mikono. 

WHO imesema ni muhimu kujenga afya bora kwa kula mlo kamili, maji ya kutosha, kufanya mazoezi na kupumzika. 

Usikubali kupotoshwa. Endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya Facebook/Twitter @NuktaFakti na Instagram @nuktafakti. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV