Hapana: Huwezi kuambukizwa Corona kwa dalili zinazoonekana pekee

November 13, 2020 1:35 pm · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Wapo watu wanaopata ugonjwa huo pasipo kuonyesha dalili zozote.
  • Upimaji ndiyo njia inayoweza kukufahamisha kama una ugonjwa huo au la!
  • Zingatia miongozo ya yote afya ikiwemo kuvaa barakoa na kunawa mikono. 

Dar es Salaam. Wakati janga la Corona likiendelea kuitesa dunia, wapo baadhi ya watu wanaaamini kuwa ugonjwa huo unasambazwa kwa dalili zinazoonekana tu na wale wasioonyesha dalili zozote hawawezi kupata maambukizi ya ugonjwa huo. 

Dalili zilizozoeleka kwa watu wanaopata ugonjwa huo aina ya COVID-19  ni pamoja na kikohozi, homa, kupumua kwa shida, maumivu ya misuli na koo, kushindwa kutambua harufu na ladha ya chakula na vitu. 

Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kuwa mtu asipoonyesha dalili hizo, siyo kwamba hana COVID-19.

Kwa mujibu wa kituo cha afya cha BeyHealth cha nchini Marekani, asilimia 80 ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huo hawaonyeshi dalili zozote na wanaweza kuendelea kuwaambukiza watu walio karibu yao wakiwemo wanafamilia na marafiki pasipo kujua. 

“Watu wenye COVID-19 wameripoti kuonyesha dalili mbalimbali zisizoonekana na zile zinazoonekana,” kinaeleza kituo hicho ambacho kinamiliki mfumo wa matibabu wa mtandaoni.


 Zinazohusiana:


Dalili zingine za ugonjwa huo ambazo hazijaripotiwa sana lakini zimekuwa zikitokea kwa watu ni pamoja na kichefu chefu, kutapika na kuharisha. 

Tunakumbushwa kuendelea kujikinga na ugonjwa huo kwa kufuata ushauri unaotolewa na wataalam wa afya ikiwemo kuvaa barakoa na kutumia tishu wakati wa kukohoa au kupiga chafya. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV