Hapana: Watu wenye VVU hawako katika hatari zaidi ya kupata Corona

December 3, 2020 8:56 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • WHO imesema dhana hiyo siyo kweli kwa sababu hakuna ushahidi wa kisayansi.
  • Wenye VVU watakiwa kuendelea kutumia dawa na kujikinga na COVID-19 kama watu wengine. 

Dar es Salaam. Wapo baadhi ya watu wanasambaza habari mtandaoni kuwa watu wenye maambukizi ya Ukimwi (VVU) au Ukimwi wako katika hatari kubwa ya kupata virusi vya homa ya mapafu vya corona (COVID-19) kutokana na changamoto mbalimbali za kingamwili wanazopitia.

Hata hivyo, wataalam wa afya wanasema hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa dhana hiyo ambayo imekuwa ikipotoshwa na baadhi ya watu wenye nia ya kuzua taharuki kwenye jamii. 

“Mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote kuwa hatari ya kupata  maambukizi ya COVID-19 ni tofauti miongoni mwa watu wenye VVU ikilinganishwa na watu wengine,” linaeleza Shirika la Afya Duniani (WHO).

WHO imeeleza kuwa mtu mwenye HIV anaweza kupata COVI-19 na akapona kama ilivyo kwa watu wengi ambao walipata maambukizi ya ugonjwa huo na wakarejea katika hali ya kawaida. 


Zinazohusiana:


Hata hivyo, kuna uwezekano wa watu wenye VVU ambao kinga zao au hawatumii dawa za kufubaza virusi (ARV) wakashambuliwa kirahisi na COVID-19 ikiwa watakutana na maambukizi hayo. 

Ili kujiweka salama zaidi, WHO imewataka watu wenye VVU kuendelea kutumia dawa za ARV kama kawaida na kupima ili kufahamu ufanisi wa kingamwili zinazotumika kupambana na magonjwa nyemelezi. 

Pia shirika hilo limewatoa hofu kuwa wanapaswa kuendelea na shughuli za kama kawaida kwa sababu wataalamu wa afya wanaendelea kutafuta kinga dhidi ya COVID-19.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
26 May, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 May, 2026
No active movers today
Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

MIKOA 5 YA KIPOLISI INAYOONGOZA KWA MAKOSA BARABARANI

Nukta TV

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

SERIKALI YAKAMILISHA MAZUNGUMZO MRADI WA LIGANGA NA MCHUCHUMA

Nukta TV

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

🔴LIVE: KAPINGA AKIWASILISHA HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA 2026/2027 BUNGENI.

Nukta TV