Dola, Euro na Pauni zaonesha mabadiliko dhidi ya Shilingi ya Tanzania
- Viwango vya ununuzi na uuzaji wa sarafu hizo vyapanda katika Benki za CRDB, NMB, huku ongezeko kubwa zaidi likirekodiwa kwenye sarafu ya Umoja wa Ulaya.
Dar es Salaam. Mwenendo wa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu za kimataifa umeendelea kuonyesha mabadiliko katika soko la fedha za kigeni, huku viwango vya ubadilishaji katika benki za biashara vikirekodi ongezeko katika baadhi ya sarafu leo, Novemba 20, 2026.
Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa leo na Benki za CRDB na NMB, Dola ya Marekani, sarafu inayotumiwa na nchi nyingi za Umoja wa Ulaya na Pauni ya Uingereza zimeonyesha mabadiliko katika bei za kununua na kuuza.
Dola ya Marekani leo kupitia Benki ya CRDB inanunuliwa kwa Sh2,615 na kuuzwa kwa Sh2,695 ikiwa ni ongezeko la Sh5 ikilinganisha na viwango vilivyotumika jana ambapo Dola moja ilinunuliwa kwa Sh2,610 na kuuzwa kwa Sh2,690.
Kwa upande wa NMB, dola inanunuliwa kwa Sh2,619 na kuuzwa kwa Sh2,699, ikiwa ni ongezeko la Sh9 katika kila kiwango ikilinganishwa na jana, ambapo ilinunuliwa kwa Sh2,610 na kuuzwa kwa Sh2,690.
Katika sarafu ya Euro, CRDB leo inanunua kwa Sh2,767.16 na kuuza kwa Sh3,067.16, ikiwa ni ongezeko la Sh12.27 kwa kila kiwango ikilinganishwa na jana, ambapo ilinunua kwa Sh2,754.89 na kuuza kwa Sh3,054.89.
NMB nayo inanunua Euro kwa Sh2,764 na kuuza kwa Sh3,059, ikiwa ni ongezeko la Sh12 kwa bei ya ununuzi, uuzaji ikilinganishwa na viwango vya jana vya Sh2,752 na Sh3,047 mtawalia.
Wakati huo huo, Pauni ya Uingereza kupitia CRDB inanunuliwa kwa Sh3,340.22 na kuuzwa kwa Sh3,640.22, ikiwa ni ongezeko la Sh2.31 katika kila kiwango ikilinganishwa na jana, ambapo ilinunuliwa kwa Sh3,337.91 na kuuzwa kwa Sh3,637.91.
NMB nayo inanunua Pauni ya Uingereza kwa Sh3,302 na kuuza kwa Sh3,654, ikiwa ni ongezeko la Sh2 katika kiwango cha ununuzi na Sh3 katika kiwango cha uuzaji ikilinganishwa Novemba 19, 2026 ambapo ilinunuliwa kwa Sh3,300 na kuuzwa kwa Sh3,651.
Mabadiliko haya yana umuhimu kwa wafanyabiashara na waagizaji wa bidhaa kutoka Marekani, Ulaya na Uingereza, kwa kuwa kupanda kwa viwango vya ubadilishaji kunaweza kuongeza gharama za malipo ya bidhaa na huduma kutoka maeneo hayo.
