Wanasayansi: Matumaini kupatikana tiba ya Ukimwi bado yapo

October 8, 2022 6:42 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni baada ya kupita zaidi ya miaka 40 tangu ugonjwa huo ugunduliwe.
  • Mpaka sasa hauna tiba. 
  • Wasema tafiti za kiyasansi zinaendelea na itapatikana miaka ijayo. 

Dar es Salaam. Licha ya kupita zaidi ya miaka 40 bila kupatikana kwa tiba kamili ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na ugonjwa wa Ukimwi, wanasayansi nchini Tanzania bado wana matumaini makubwa kuwa tiba itapatikana kwa ikiwa tafiti za kisayansi zitaimarishwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) mlipuko wa Ukimwi ulianza miaka ya 1980 duniani na kuua maelfu ya watu.

Tangu kuanza kwa janga hili, watu milioni 84.2 wameambukizwa virusi vya Ukimwi na takriban milioni 40.1 wamekufa kwa VVU hadi kufikia mwaka 2021, WHO inaeleza. 

Shirika hilo linaeleza zaidi kuwa watu milioni 38.4 walikuwa wakiishi na VVU mwishoni mwa 2021.

Inakadiriwa kuwa asilimia 0.7 ya watu wazima wenye umri wa miaka 15 hadi 49 duniani kote wanaishi na VVU, ingawa mzigo wa janga hili unaendelea kutofautiana kwa kiasi kikubwa kati ya nchi na mabara.

Afrika ndiyo inatajwa kuathirika zaidi, ambapo karibu mtu 1 kwa kila watu wazima 25 (3.4%) anaishi na VVU na ni zaidi ya theluthi mbili ya watu wanaoishi na VVU duniani kote.

Tangu ugonjwa huo uanze kutikisa dunia, wanasayansi na wataalam wametumia muda wao mwingi kufanya tafiti ili kupata tiba lakini bado hawajafanikiwa. 

Ili kujikinga na ugonjwa huo, watu wanashauriwa kutumia njia mbalimbali kujikinga ikiwemo kondomu, kuepuka ngono zembe na waliopata maambukizi kutumia dawa za kufubaza virusi (ARV). 

“Hakuna tiba ya maambukizi ya VVU. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa upatikanaji wa kinga bora ya VVU, utambuzi, matibabu na matunzo, ikiwa ni pamoja na magonjwa nyemelezi, Ukimwi umekuwa hali ya kiafya inayoweza kudhibitiwa, inayowezesha watu wanaoishi na VVU kuishi maisha marefu na yenye afya,” imeeleza WHO. 

Licha ya kuwa Ukimwi bado unawatesa watu duniani, kuna uwezekano mkubwa wa tiba kupatikana siku zijazo. Picha| International AIDS Society. 

‘Tumaini bado lipo’

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la DARE, Dk Lilian Mwakyosi anasema licha ya kupita muda mrefu bila kupatikana kwa tiba kamili ya Ukimwi, bado Watanzania wanapaswa kuwa na matumaini kuwa hilo suala linawezekana.

“Kuna matumaini ya kupata tiba ya Ukimwi kupitia tafiti za kisayansi,” anasema Dk Mwakyosi, wakati wa warsha ya siku moja kuhusu uelewa wa tafiti za tiba ya Ukimwi iliyofanyika jijini Dar es Salaam wiki hii. 

Mwanasayansi huyo anaamini kuwa inawezekana kutibiwa Ukimwi na mtu akapona siku zijazo kwa sababu tafiti za kisayansi na kitabibu zinaendelea kwa kutumia mikakati mbalimbali. 

Kuna mikakati mitatu mkuu inayochunguzwa. Kila moja inachukua mtazamo tofauti kwa changamoto ya kimsingi ya maambukizi ya VVU na uwezo wake kujificha katika seli ambazo hazifanyi kazi (pia huitwa seli za kupumzika) na zisizogawanyika. 

Tiba yenye ufanisi italazimika kuondoa hifadhi hizi za virusi au kuhakikisha kuwa virusi vilivyoamilishwa haviwezi kurejesha maambukizi mwilini.


Mshtuko na kuua

Mkakati huu wa hatua mbili unalenga kuondoa (au kushtua) virusi kutoka kwa seli zilizopumzika kwa dawa ya kurudisha nyuma muda wa kusubiri na kisha kufuatilia uingiliaji kati mwingine ili kuua seli zilizoambukizwa.


Zinazohusiana:


 

Tiba ya jeni/udanganyifu

Baadhi ya mikakati ya kubadilisha seli ili VVU isiweze kuziambukiza inahusisha kuhariri jeni ili kuondoa kipokezi cha protini kinachojulikana kama CCR5 (mlango ambao VVU hutumia kuingia kwenye seli za CD4+ T). 

Njia nyingine hurekebisha seli za kinga ili kutambua vyema seli zilizofichwa zilizoambukizwa katika mwili. 

Watafiti wanafanya kazi katika kutengeneza mbinu ya kutoa teknolojia ya uhariri wa jeni moja kwa moja kwenye mwili bila kuondoa seli. Hivi sasa, urekebishaji wote wa jeni unahusisha kutoa seli za kinga kutoka kwa watu walio na VVU, kuzirekebisha na kisha kuzirudisha kwa mtu.

Changamoto ya tiba hii ni kuwa ni vigumu kukusanya seli za kinga zilizoambukizwa VVU, na hakuna anayejua idadi ya jeni zilizobadilishwa zinazohitajika kufikia matokeo.


Urekebishaji wa kinga

Vidhibiti vya kinga hurejelea aina yoyote ya dawa au utaratibu unaosababisha aina fulani ya mabadiliko endelevu katika mfumo wa kinga ili kupambana vyema na VVU. 

Urekebishaji uliofanikiwa wa kinga unaweza kutambua seli fiche zinazoshikilia virusi kabla ya seli kuamshwa upya, na kuimarisha uwezo wa kuua VVU mara tu mgawanyiko wa seli unapoanza tena.

Dk Mwakyosi anasema tafiti za tiba ya Ukimwi zinazidi kupanuka, na aina mbalimbali za majaribio yaliyopangwa yanayoendelea duniani. majaribio.


Tangazo:


Kwa nini tiba imechelewa?

Akizungumzia sababu za tiba ya ugonjwa huo kuchelewa kuvumbuliwa, amesema virusi vya Ukimwi vimekuwa vikibadilika badilika mara kwa mara na hivyo kuwapa wakati mgumu watafiti kutoa tiba (chanjo au dawa) ambayo itaweza kuwa mbadala.

“Tafiti hizi ni gharama zinahitaji pesa nyingi kuzikamilisha,” anasema mtaalam huyo na kuongeza kuwa anuia za virusi vya Ukimwi hutofautiana kutoka eneo moja hadi lingine.

“Kupata tiba ya Virusi vya Ukimwi ni ndoto ya mwisho. Ingawa hatua hii bado ni ngumu na kazi kubwa zaidi inahitajika, inatupa matumaini makubwa kwa siku za usoni tunaweza kuumaliza Ukimwi kwa njia za sayansi kupitia chanjo au tiba,” alisema mwaka 2019, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Ukimwi (UNAIDS), Michel Sidibé.


Nini kifanyike?

Dk Mwakyosi anasema kupitia DARE wataendelea kutoa hamasa na kushirikisha makundi mbalimbali kwenye jamii wakiwemo watalaam wa afya na viongozi wa dini juu ya uelewa wa tiba ya Ukimwi na hatua zinazochukuliwa kutafuta tiba kamili ya ugonjwa huo.

Ikiwa watu watapa uelewa zaidi kuhusu ugonjwa huo, itasaidia kupunguza idadi ya watu wanaopata maambukizi wakati wakisubiri wanayasansi kutumia uwezo wao kutafuta tiba.

Sera ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi ya mwaka 2001, nayo inahimiza kufanyika kwa tafiti mbalimbali kuhusu ugonjwa huo na tiba kwa kushirikisha wataalam wa ndani na nje ya nchi. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV