Fahamu haya unaponunua ‘mouse’ ya kompyuta
- Mbali na ukubwa, ni muhimu kuzingatia uimara wa kifaa hicho.
- Hakikisha ununua ‘mouse’ ambayo betri zake zinapatikana kirahisi.
- Hakikisha inaendana na ukubwa wa kiganja cha mkono wako.
Dar es Salaam. Kwa baadhi ya kazi zinazofanywa na kompyuta, matumizi ya “mouse” hayaepukiki ili kupata motokeo mazuri.
Kwa ambao hawaelewi “mouse” ni nini, kwa urahisi ni kifaa kinachotumika sambamba na komyuta ambacho kinakusaidia kubonyeza, kusogeza na kuchagua nyaraka mbalimbali kwenye kompyuta yako.
Kuna mengi ya kuzingatia unapununua kifaa hicho. Ni mambo gani mengine uzingatie? Jifunze zaidi.
Nunua ‘mouse’ isiyopiga kelele
Pata taswira ya hii, upo katika ofisi na watu wote wanatumia mouse na zote zinatoa sauti ukizibonyeza. Bila shaka umeelewa kitu kinachoongelewa.
Endapo unaenda kununua bidhaa hiyo, ijaribu uone kama inatoa sauti au laa!.
Karim Salkim ambaye ni mbunifu wa grafiki, amesema zipo baadhi ya kazi hazihitaji kelele, hivyo uchaguzi wa mouse nzuri utakusaidia kupunguza usumbufu usio wa lazima.
Endapo ukishindwa kufahamu masuala muhimu kuhusu ‘mouse’ omba ushauri kwa ndugu na wataalamu wakuelekeze. Picha| Rodgers George.
Hakikisha inaendana na kiganja cha mkono wako
Hauhitaji kifaa ambacho hauko huru nacho kwani kitakupunguzia ufanisi pale unapofanya kazi. Kwa kuwa ‘mouse’ huja katika ukubwa tofauti, hakikisha unanunua inayoendana na kiganja cha mkono wako.
Bila kufanya hivyo, unaweza kujikuta unanunua ‘mouse’ kubwa au ndogo kiasi cha kushindwa kuifurahia.
Soma zaidi:
- Hivi ndivyo unavyoweza kupata simu mpya kwa bei rahisi
- Jinsi ya kusafisha kiandikio cha kompyuta yako
- Simu unazoweza kununua kwa bei chini ya Sh1 milioni
Upatikanaji na aina ya betri zinazotumika
Kuna ‘mouse’ zinazotumia betri mbili, zipo zinazotumia betri moja. Lakini zipo ambazo zinatumia betri kubwa au ndogo.
Ili kuepukana na usumbufu, unashauriwa kununua mouse ambayo betri zake hazitokusumbua katika kuzipata, ikiwa ulizonazo zitaishiwa nguvu.
“Unaweza kuwa unanunua ‘mouse’ ya kazi na kazi zako unafanyia kijijini au mbali na miji, kama betri za mouse yako hazipatikani kiurahisi, itakupa tabu mbeleni,” ameeleza mdau wa teknolojia jijini Dar es Salaam, Sise Christopher.
Uimara wa kifaa hicho
Kwa kuwa kifaa hicho kimetengenezwa kutosheleza mkononi, kisipotunza vizuri kinaweza kuharibika mapema. Lakini kuharibika hutegemea na uimara wa kifaa husika.
Hakikisha unanunua ‘mouse’ imara hata kama inauzwa kwa bei ya juu ili idumu mapema. Lakini jukumu la kukifanya kifaa hicho kidumu muda mrefu liko mikononi mwako.
Latest
