Fahamu jinsi ya kutumia miwani janja (Smart glasses)
- Iliingizwa sokoni kwa mara ya kwanza mwaka 2013 na kampuni ya google.
- Inaweza kufanya kazi zaidi ya moja kwa muda mchache.
Arusha. Miwani janja ni aina mpya ya miwani iliyoambatanishwa na teknolojia mbalimbali za kidijitali kama kamera, spika ndogo, skrini ndogo (hud), au sensa, inayowezesha kufanya mambo zaidi ya kuona tu.
Fikiria dunia mpya ambayo hauhitaji tena kubeba simu ya mkononi bali shughuli zote muhimu kama kuwasiliana, kurekodi picha na video, kusikiliza muziki, kuonesha ramani, kufuatilia hali ya afya (health monitoring) na nyingine nyingi zinawezeshwa na kifaa kidogo.
Miwani hiyo iliingizwa sokoni kwa mara ya kwanza na kampuni ya Google kupitia kifaa cha Google Glass na kuanza kusambazwa kwa kwa majaribio mwaka 2013 na kuuzwa kwa Dola za Marekani 1,500 (Sh3.7 milioni).
Kwa sasa kifaa hicho kinapatikana katika tovuti za manunuzi mtandaoni kama eBay na Amazon kwa bei ya Sh248,579 hadi Sh6.4 milioni (Dola za Marekani 100 hadi 2,600).
Jinsi ya kutumia miwani janja
Ikiwa utanunua kifaa hicho, matumizi yake ni rahisi sana ambapo hatua ya kwanza kabla hujaivaa inatakiwa kuwa ni kusoma mwongozo maalum unaopatikana ndani ya boksi au pamoja na bidhaa hiyo.
Kila smart glasses ina sifa tofauti, baadhi zina kamera, za kupiga simu, za kuonyesha taarifa (AR), au za kuunganisha na simu kupitia Bluetooth hivyo mwongozo wa mtumiaji ili kuelewa jinsi ya kuzima, kuwasha, na kutumia features hizo.

Miwani janja inaweza kuvaliwa na jinsi zote (Mwanaume au mwanamke) kwa ajili ya matumizi mbalimbali.Picha/ Amazon.
Andaa miwani yako
Kwa mujibu wa tovuti ya Huawei Eyewear, kabla ya kutumia smart glasses, hakikisha zimechajiwa kikamilifu ili uzitumie kwa muda mrefu bila usumbufu wa kuzichaji mara kwa mara.
Jinsi ya kuchaji hutofautiana kati ya kampuni na kampuni, ila unaweza kutazama kama kuna betri na uunganishe miwani na waya maalum wa kuchaji kisha utazame kama inaingiza umeme kupitia taa za rangi ya kijani au nyekundu zilizopo pembeni ya miwani.
“Usichaji miwani ukiwa umeivaa, usiipige au kuvuta chaja kwa nguvu kupita kiasi, miwani itajizima ikiwa haitatumika kwa zaidi ya dakika tatu na itawaka automatiki unapovaa au unapochaji,” imesema tovuti ya Huawei.
Washa na uunganishe na vifaa vingine
Unaweza kutumia kifaa hicho cha kisasa kwa kukiwasha kisha kuiunganidha na vifaa vingine muhimu ikiwemo simu ya mkononi na kompyuta kupitia ‘Bluetooth’ ili uweze kupokea taarifa, kupiga simu, au kupakua programu tumizi (app) zinazohitajika.
“Anza kwa kuwasha miwani (bonyeza na ushikilie kitufe cha kuwashia kwa sekunde 3–5) kisha fungua programu kwenye simu yako na uchague sehemu ya kuunganisha kifaa kipya (Pair New Device).
…Thibitisha nambari ya uthibitisho itakapoulizwa na kifaa chako kitakuwa tayari kwa matumizi,” inaeeleza tovuti ya masuala ya teknolojia ya Hotus Projector.
Hata hivyo tovuti ya Hotus imebainisha kuwa baadhi ya miwani hususani inayotumia teknolojia ya AR inaweza kuhitaji huduma ya intenti (Wi-Fi) au akili bandia kufanya kazi ipasavyo.

Mbali na kurahisisha shughuli za kidigitali, miwani janja inaweza kutumiwa pia na watu wasioona.Picha/Matt. elly.
Fanya matengenezo ya msingi na ujifunze kuitumia
Baada ya kuunganisha, weka wasifu wako ikiwemo email, namba ya simu kisha weka ukubwa wa maandishi, sauti, mwangaza wa kioo unaoupendelea pamoja na vipengele binafsi vitakavyokuwezesha kuitumia kikamilifu.
Pamoja na kunganisha masuala hayo unatakiwa kujifunza kutumia ishara mbalimbali ili uweze kuitumia kwa urahisi zaidi kwa sababu Smart glasses nyingi zinatumia mfumo wa kugusa au sauti ili kufanya kazi.
Mambo ya kuzingatia
Pamoja na urahisi na umuhimu wa kutumia kifaa hicho katika zama hizi za kigitali tovuti ya Huawei Eyewear inashauri kukitumia kwa uangalifu ili kuweza kulinda macho, na masikio kutokanana sauti.
“Ili kulinda usikivu wako, usisikilize sauti kwa sauti ya juu kwa muda mrefu., usipashe joto au kuinamisha mikono ya kioo ili kuepuka uharibifu, kushindwa kufanya kazi na hatari za moto.
…Kuvaa kifaa hiki hakutalinda macho yako kutokana na majeraha ikiwa unatazama moja kwa moja jua au vyanzo vingine vya mwanga mkali,” imeongeza tovuti ya Huawei.
Pamoja na hayo imeshauiriwa kutumia kitambaa lain kuisafisha miwani janja hiyo na kuweka mbali na jua au watoto ili kupeuka uharibifu wowote unaoweza kujitokeza.
Latest