Jinsi ya kusafisha kiandikio cha kompyuta yako

November 10, 2020 1:13 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni sehemu ya kuandikia maandishi yanayojitokeza kwenye skrini ya kompyuta (Keyboard).
  • Sehemu hiyo hupata uchafu hasa inapotumia kwa muda mrefu.
  • Kuisafisha, unahitaji kitambaa na dawa maalumu.

Dar es Salaam. Usafi wa kompyuta huenda siyo kipaumbele kwa watu wengi lakini zana hiyo pia inahitaji kufanyiwa usafi ili kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi.

Pale kompyuta yako inapokuwa imechafuka kwa vumbi ina uwezekano wa kupata changamoto za kiufundi ikiwemo kupungua kwa ufanisi wa feni inayotumika kupoza kompyuta yako.

Leo tutazungumzia jinsi ya kusafisha kiandikio cha kompyuta yako (Keyboard) kwa usahihi.

Kabla ya kuendelea,  ni muhimu kufahamu kuwa kwa mujibu wa Shirika la Habari la The Verge, keyboard yako inaweza kuwa na uchafu unaoonekana na usioonekana kutokana na kutumika kwa kufanyia kazi za ofisi, kuwsiliana na watu na hata kwa ajili ya burudani ikiwemo michezo ya video kidijitali (video games).

Endapo unahangaika na uchafu wa vumbi, nywele, michanga na mwingineo, hizi ndizo njia sahihi za kuisafisha keyboard yako.

Zima komputa yako

Kabla ya kuanza kusafisha ni vyema kuizima kompyuta yako ili kuepusha changamoto zaidi ikiwemo kupigwa shoti endapo maji maji yataingia kwenye kompyuta. 

Ondoa uchafu unaoonekana ukiwemo mchanga

Kufanya hivyo, geuza kompyuta yako kwa muelekeo wa chini juu na kisha acha ufafu udondoke. Unaweza kuipiga kidogo sehemu ya chini ya kompyuta yako ili kudondosha uchafu mwingine uliokataa ndani.

Pia, endapo mfuko wako unaruhusu, unaweza kununua kifaa maalumu cha kusafishia vumbi la keyboard kinachojulikana kama “press cleaning slime” ambacho hupenya hadi chini ya vitufe (button) vya keyboard yako kutoa vumbi na uchafu mwingine kutokana na kuwa katika hali ya ujiuji liogandiana. 

Kifaa hicho hugandiana na uchafu pamoja na vumbi na kuacha keyboard yako ikiwa safi.

“Press cleaning slime” ambacho hupenya hadi chini ya vitufe (button) vya keyboard yako kutoa vumbi na uchafu mwingine. Picha| HGTV.

Pia, kama una mashine ya umeme ya kuvuta uchafu (Vaccum cleaner) unaweza kuitumia lakini hakikisha unatumia kasi ya chini zaidi ili usiishie kuharibu keyboard yako. 

Mashine ya kukausha nywele (blow dryer) nayo unaweza kutumia lakini kwa tahadhari ili usiharibu vifaa vya ndani ya kompyuta.


Soma zaidi


Tumia dawa maalumu kusafisha keyboard yako

Baada ya kuondoa uchafu unaoonekana kwa macho, sasa ni wakati wa kuondoa bakteria na uchafu mwingine usioonekana kwa macho.

Kwa mujibu wa The Verge, unaweza kuanza kwa kutumia kitambaa kisafi kisichoacha nyuzi nyuzi baada ya kufuta, dawa maalumu ya kusafishia keyboard na kisha kusafisha kitufe kimoja hadi kingine.

Katika hatua zote za usafi, usipulizie kimiminika chochote juu ya keyboard yako. Hakikisha unatumia kitambaa kikavu na unapotumia dawa, ipulizie kwenye kitambaa na siyo kwenye keyboard.

Baada ya hapo, furahia kutumia kompyuta yako ikiwa safi na yenye kuvutia hata katika macho yako.

Enable Notifications OK No thanks