Usidanganyike: Haya siyo madhara ya chanjo ya Corona

December 19, 2020 8:14 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni madai kuwa “mgonjwa wa Corona aliyepata chanjo kaanza kutafuna wagonjwa wengine”
  • Habari hiyo si ya kweli kwani imetumia picha ya kijana aliyekufa baada ya kupigwa risasi tatu kifuani Marekani mwaka 2019.
  • Mpaka sasa hakuna madhara ya chanjo dhidi ya Corona yaliyoripotiwa.

Dar es Salaam. Kama wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii hasa WhatsApp, huenda umekutana na habari inayoelezea madhara yanayotokana na chanjo dhidi ya ugonjwa Corona.

Habari (Breaking News) hiyo ambayo iko kwenye mfumo wa picha inaonyesha chumba cha upasuaji katika moja ya hospitali nchini Marekani kikiwa kimetapakaa damu baada kutokea kwa fujo za wagonjwa wanaodaiwa kutumia chanjo ya COVID-19.

Nukuu ya habari hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kiingereza inasema “Hospitals on lockdown as first covid vaccine patient starts eating other patients” ikimaanisha kuwa “Hospitali zafungwa baada ya mgonjwa wa kwanza kupewa chanjo ya Corona kuanza kula wagonjwa wengine”.

Habari hiyo haina ukweli wowote na inalenga kupotosha watu wasitumie chanjo dhidi ya Corona.

Ukweli huu hapa

Nukta Fakti imefanya utafiti kutumia zana ya “TinEye” na kubaini kwamba picha iliyotumika kwenye habari hiyo ilipigwa Februari 14, 2019. 

Lilikuwa ni tukio la kijana mmoja Marekani aliyefika hospitali ya Chuo Cha Temple Marekani na risasi 3 kifuani baada ya manesi na wauguzi kujaribu kumsaidia kwa kuzitoa risasi hizo mwilini mwake.


Zinazohusiana:


Baada ya zoezi la kuokoa maisha ya kijana huyo kufanyika bila mafanikio, kitanda kilichotumika kumfanyika upasuaji kiliwekwa mbali na damu nyingi kubaki zikizagaa chini.

Hata hivyo, baadhi ya watu wasio na nia njema, wametumia picha hiyo kutengeneza habari ya upotoshaji ili kuzuia juhudi za Serikali na mashirika ya kimataifa likiwemo la afya (WHO) za kupambana na Corona. 

Mpaka sasa, WHO haijatoa tamko lolote kuhusu madhara ya chanjo ya Corona ambayo imeanza kutumiwa katika nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza na Marekani.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW