Filamu ya Black Widow: Sababu kwanini usikimbie matatizo yako

July 9, 2021 3:04 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Pale teknolojia inapochochea usaliti na chuki, ndugu wawili wanangudua ukweli unaoumiza.
  • Ukweli huo haufui dafu baada ya ndugu hao kuamua kushikana kwa dhiki na faraja.
  • Usaliti, maumivu ya moyo na mafunzo ya maisha ni sehemu ya filamu ya Black Widow.

Dar es Salaam. Huenda kuna mtu unataka umuangamize lakini kila ukijaribu, ni kama mtu huyo anakuwa hatua moja mbele yako kwani pale unapodhani umefuta historia yake, siku mbili unasikia yupo sehemu fulani.

Unaweza kukumbuka sura yake kutokana na umaridadi aliouonyesha katika filamu ya “The Avengers” huku akipigana upande kwa upande na Hulk, Captain America na wengine kibao wanaotengeneza familia hiyo.

Baaada ya kumwona katika hadithi ambazo alikuwa tayari katika mafanikio, Natasha Romanoff sasa anakuja na historia yake katika filamu ya Black Widow.

Historia hii inaturudisha kipindi mwanamama huyo alichagua kile dunia inataka awe badala ya kile ambacho ameumbwa kufanya. Visasi, mauaji na kusahau wajibu wake ni kati ya mambo ambayo yameendelea kumfukuzia kila siku lakini hata hivyo kwa sasa hayuko tayari tena kuendelea  kukimbia historia yake.

Black widow na familia

Kabla ya kuwa mwanadada mahiri katika familia ya Avengers, Romanoff  alikuwa na majukumu kama walivyo watu wengine.       

Alikuwa na familia yenye mdogo wake wa kike aliyemtazamia kwa kila kitu. Ulinzi, mfano wa kimaisha na tumaini ni kati ya vitu ambavyo Romanoff alishindwa kuvionyesha kwa mdogo wake Yelena Belova.

Mwanzo upo hivi, wazazi walezi wa mabinti hao, Alexei Shastacov na Melina Vostokoff wanawahamishwa kutoka mahali walipokuwa wakiishi zamani baada ya kupata “mission” (kazi) inayotenganisha familia hiyo ambayo wote walitamani iwe familia ya kweli.

Mabinti hao wanawekwa kwenye programu ya Red Room ambayo kazi yake kuu ni kuzalisha vikosi vya wapelelezi waliofundishwa wakabobea. 

Hata hivyo, Romanoff anatoroka na kukimbilia Romania baada ya kuvunja baadhi ya sheria alizotakiwa kuziangazia. Anakuwa ametengana na mdogo wake.

Ifahamike kuwa, wakati wakiwa kwenye mafunzo ya Red Room, wawili hao waliwekewa vitu pasipokujua, vitu ambavyo vilimwezesha mkuu wa programu ya Red Room, Dreykov kuwaendesha bila hata ufahamu wao.

Ni kama umepanga kufanya kitu hiki lakini unajikuta umefanya kingine bila hata wewe kujijua. Ndicho kitu ambacho Dreykov alifanya kwa wanawake wote waliopitia programu ya Red Room iliyozalisha wanawake wapelelezi waliojulikana kama “Black Widows”.

Shabaha za mishale ya kuteketeza zinavyolengwa huku mapanga na visu vikiwa silaha dhidi ya wanadamu na siyo mboga tena. Picha| Dare Daniel.

Mwanzo wa njiapanda ya familia

Wakati Romanoff akiendelea na maisha yake, Mdogo wake Belova aliendelea kufanyia kazi Red Room. Naye anaingia mkenge baada ya kumuua black widow mmoja ambapo anagundua kitu kinachoitwa “Red Dust”, vumbi linaloweza kuondoa uwezo wa Dreykov kukuendesha. 

Kwa mahaba na dada yake, Belova analituma vumbi hilo kwa dada yake akiwa na matumaini ya kuwa Romanoff atakuja kumuokoa.

Belova anasubiri, anasubiri, jua linachomoza, jua liazama lakini Romanoff hatokei badala yake alikimbia na vumbi hilo na kuishia katika mapambano na  Taskmaster, aliyetumwa na Dreykov kurudhisha vumbi hilo kwenye mikono sahihi.

Kupitia maelezo hayo, ni wazi umegundua kuwa mabinti hao wawili wanatafutwa na kundi ambalo wameliumiza. Romanoff ambaye amejaribu kumuua Dreykov na mwanaye, na Belova ambaye ameua mmoja wa Black widows.

Safari iliyojaa usaliti, kumbukumbu zinazoumiza na uhalisia usioweza kupingika, ni sehemu ya visa utakavyokutana navyo kwenye filamu hii ya Black Widow.

Visasi, kujimwambafai na kutaka kuonyesha dunia ya kuwa watu wote wapo kwenye mikono ya mtu mmoja, ni sehemu ndogo sana ya Black Widow. Shuhudia mkono wa mauaji unavyojipambanua.

Shabaha za mishale ya kuteketeza zinavyolengwa huku mapanga na visu vikiwa silaha dhidi ya wanadamu na siyo mboga tena.

Unaweza kuitazama filamu hii kupitia kumbi za kuangalizia filamu kwa gharama ya hadi Sh10,000 tu ili kujua hatma ya dada na mdogo wake walivyojaribu kuukimbia msumeno wa mamlaka.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Rais Samia azindua minara 758, aacha maagizo mazito juu ya mkongo wa taifa

Nukta TV

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

JAJI MKUU: Njia za asili ni mojawapo ya njia halali za utatuzi wa migogoro

Nukta TV

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Hesabu ya bosi, bei ya mafuta pasua kichwa madereva wa daladala

Nukta TV