Utafanya nini mume wako akiuwawa na magaidi? Filamu ya “Army of One” itakufunza mengi

January 9, 2021 7:25 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Inamhusu mwanamama anayerudi kulipa kisasi kwa waliomuua mume wake.
  • Ni baada ya yeye na mumewe kuingia kwenye nyumba ambayo hawakupaswa kuingia.
  • Hata pale mwenye nyumba anapoamua kuwaua, anashindwa kufanya kazi nzuri kwa mwanamama ambaye anarudi kumsaka.

Dar es Salaam. Ni swali kwa wanawake wote wanaosoma makala hii. Utafanya nini pale magaidi watakapomuua mume wako mbele ya macho yako na kukuacha wewe ukiwa hai?

Huenda wengi watauzika mwili wa aliyekuwa mume wao na kuomboleza na kuendelea na maisha yao.

Kwa mwana dada Ellen Hollman (Brenner) kamwe hawezi kuishia hapo.

Akiwa matembezini na mume wake Matt Passmore (Dillion) wawili hao wanafurahia muda wao wa mapumziko au watu wengi huuita “vacation”. 

Pale mvua inaponyesha wakati wakiwa msituni, wanakimbilia kwenye nyumba ambayo wanaamua kujisitiri licha ya mmiliki kutokuwepo. 

Wapo wawili tu katika nyumba nzima, unafikiri wanafanya nini? Na pale wanapojisikia wapo nyumbani zaidi, wanaanza kutalii kwenye mjengo wa watu. Hapo ndipo mkasa wote unapoanzia.

Dillion na mkewe Brenner wanaingia katika chumba ambacho kina bunduki zinazotosheleza kutumika kwenye vita ya kwanza ya dunia na hapo ndipo wanapogundua kuwa wapo kwenye nyumba ya magaidi.

Wanapogundua kuwa suluhu iliyopo ni kuondoka katika nyumba hiyo, wanakuwa wamechelewa kwani mwenye nyumba anawasili na siyo rafiki kama walivyodhani. 

Wakati wanahamaki, wote wanakula kipigo na kupoteza fahamu na wanapozinduka, wanajikuta kwenye kipindi cha mahojiano.


Soma zaidi:


Pale yote yanapoenda kombo na majambazi wanapogundua kuwa wawili hao ni wadau wa vyombo vya dola, wanabaki na chaguo moja la kuwauwa. 

Hata hivyo, huenda kazi yao haikuwa madhubuti kwa kumuua Brenner kwani, moyo wake bado unadunda.

Wanapotupa miili ya wawili hao, Brenner anaamka na kuufunika mwili wa mume wake na kurudi kulipiza kisasi.

Je, mkono wake utaweza kukabiliana na wa magaidi? Atafanikiwa kulipiza kisasi kwa waliomtia mume wake mauti? Jibu maswali yako kwa gharama ya Sh10,000 kupitia kumbi za kuangalizia filamu za Century Cinemax zilizopo katika maduka makubwa (malls) yakiwemo Mlimani City, Aura na na Dar Free Market (DFM) jijini Dar es Salaam. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV